Anayetakiwa: Gareth Bale (kushoto) amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid na sasa Manchester United
KLABU ya Manchester United inaweza kugeuzia mawingo yake kwa Gareth Bale baada ya kumkosa mmoja wa wachezaji iliyokuwa inawataka sana.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu wameshuhudia kiungo wa kimataifa wa Hispania chini ya umri wa miaka 21, Thiago Alcantara wa Barcelona akichagua kumfuata kocha wake wa zamani, Pep Guardiola klabu ya Bayern Munich.
Lakini United imedhamiria kumpa sapoti kocha wake mpya, David Moyes katika harakati zake za kuunda kikosi cha kutetea taji kwa kumnunulia winga wa Tottenham, Bale, ambaye alishinda tuzo tatu za Mchezaji Bora wa Mwaka msimu uliopita baada ya kufunga mabao 21 Spurs.Ameota mbawa: United ilikuwa inamtaka Thiago Alcantara (katikati), ambaye amesaini Bayern Munich
Beki kinda wa Uruguay, Guillermo Varela ni mchezaji pekee aliyesajiliwa na United majira haya ya joto, lakini klabu hiyo inaweza kuanza mpango wa kumsajili kwa Pauni Milioni 60 Bale mwezi huu, kwa mujibu wa Daily Mirror.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.