FEZA WA TANZANIA AGONGANISHA MABWANA BAADA YA KUINGIA KUONGA NA NJEMBA IKIWA UCHI BAFUNI (BBA THE CHASE)

clip_image001Shemeji yetu Mbotswana, Oneal amechukizwa na kitendo cha Feza Kessy kwenda kuoga na mwanaume mwingine.
Jana jioni, Feza ilimlazimu amuombe msamaha mpenzi wake huyo aliyeoneshwa kuumizwa roho na kitendo hicho.
“Umefanya tena leo asubuhi. Umeniacha kitandani na kwenda kuoga na mwanaume aliye UCHI. I was so disappointed”, alisema Oneal ambaye hata hivyo hakumtaja mwanaume huyo.
“What was wrong with this particular shower”, aliuliza Feza ambaye alijibiwa na Oneal,”He was naked”.

Wasiwasi wa Oneal ni kama vyombo vya habari vya Tanzania vikipata picha hizo zinazomuonesha Feza akioga na mwanaume mwingine bafuni na kuzitumia, jambo ambalo linaweza kutia doa mapenzi yao.
Mrembo huyo wa Tanzania alimuomba msamaha mpenzi wake na kisha kumkumbatia na kumbusu huku wakijifunika shuka gubigubi, kitu kilichomaliza hasira za Mtswana huyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post