Unknown Unknown Author
Title: MAMA SALMA AWATAKA WAKAZI WA LINDI KUISHI KWA UPENDO NA USHIRIKIANO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Shehe na Kadhi Mkoa wa Lindi Al Haj Mohamed Said Mshangani baada ya kufuturu nyumbani kwa Mama S...

mama jk futariMke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Shehe na Kadhi Mkoa wa Lindi Al Haj Mohamed Said Mshangani baada ya kufuturu nyumbani kwa Mama Salma Lindi Mjini hapo janamama jk ldBaadhi ya wananchi wa Lindi Mjini walioalikwa kufuturu nyumbani kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakisikiliza mawaidha yaliyokuwa yakitolewa baada kufuturu.mama jk ld 2Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadhi ya akina mama aliofuturu nao nyumbani kwake Lindi Mjini jana jioni.

(picha zote na John Lukuwi)

Na: Abdulaziz video
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa mkoa wa Lindi kuishi maisha ya upendo, ushirikiano, umoja na kuwasaidia watu
wasiojiweza kwa kufanya hivyo watapata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Mama Kikwete ametoa wito huo jana wakati wa futari ya pamoja
iliyowajumuisha watu wa makundi mbalimbali kutoka mkoa huo.
Mama Kikwete alisema upendo ukiwepo ndani ya jamii watu wataishi
maisha ya furaha na amani huku wakisaidiana kwa kupeana vitu vichache walivyonavyo.

‘Tuwe watu wa kuishi maisha ya kumpendeza Mwenyezi Mungu siyo wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani peke yake bali katika maisha yetu yote, tusali swala tano na kuamka usiku wa manane muda ambao Dunia imetulia, kila mtu anakuwa amelala.

Muombe Mwenyezi Mungu akuamshe muda huo ili uweze kusali bila kusahau kumshukuru kwa kukupa uhai na umri uliofikia na hata kama utakufa muda huo hautakuwa na hofu kwani umeshatengeneza mahusiano yako na Mungu”, alisema Mama Kikwete.

Aliendelea kusema ni muhimu kwa muumini wa dini ya Kiislamu kukumbuka kusali, kufunga na kusaidia watu wenye mahitaji maalum kwa kufanya hivyo atakuwa anajilinda na kujitengenezea maisha mema pindi atakapokufa.

Mama Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kutunza amani ya nchi na
kuwataka wakazi wa mkoa huo wanapokuwa kwenye mikusanyiko mbalimbali ikiwa ni pamoja na misikitini, makanisani kwenye sherehe na misiba wahubiri umuhimu wa amani kwani mahali penye vita hakuna umoja, ushirikiano na upendo.

Hivi sasa waumini wa dini ya Kiislamu wako katika kumi la pili la
kufunga ambalo ni la msamaha kama alivyosema Mtume Swalallahu Alayhi Wassalam (S.A.W) hivyo basi kwa wale wanaofunga wanatakiwa kujikita zaidi kufanya mambo mazuri kwa watu ikiwa ni pamoja na kulisha wengine kwani ukimpa kula na kunywa mwenzako Mwenyezi Mungu anakulipa zaidi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top