Unknown Unknown Author
Title: WARSHA YA WADAU WA MPINGO KUFANYIKA KILWA TAREHE 30/07/2013
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Gasper Makala ,Mkurugenzi wa shirika la Mpingo.(.MCDI) Na. Abdulaziz Video, Kilwa Shirika la Mpingo(MCDI) Limeandaa Warsha ya Wadau wa Shi...

IMG_0998Gasper Makala ,Mkurugenzi wa shirika la Mpingo.(.MCDI)IMG_0973

Na. Abdulaziz Video, Kilwa

Shirika la Mpingo(MCDI) Limeandaa Warsha ya Wadau wa Shirika hilo itakayofanyika hapa wilayani kilwa katika Mji mdogo wa Kilwa Masoko tarehe 30/07/2013. katika Ukumbi wa Hotel ya PEC Maarufu kwa Sultan kuanzia saa mbili kamili asubuhi.

Lengo kuu la warsha hiyo ni Kujadiliana na kukubaliana jinsi gani Shirika hilo la Mpingo liendelee kutoa huduma kwa jamii katika Kusimamia Misitu ya Vijiji kiuendelevu pasipo kutegemea wafadhili kwa kiwango kikubwa.
Akizungumzia Warsha Hiyo,Mkurugenzi wa shirika hilo ,Gasper Makala alibainisha kuwa warsha hiyo itakayoshirikisha Wakuu wa Wilaya za Rufiji, Nachingwea na wenyeji Kilwa pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri, Wabunge na Madiwani watahudhuria Kwa pamoja na Wawakilishi wa Vijiji pia wawakilishi wa wafadhili Ubalozi wa Norway na Finland

Kwa upande wa shirika la Mpingo(MCDI)pia litawakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi na wajumbe wake na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila atakuwa Mgeni rasmi

Mwaka 2008 mashirika 10 yasiyo ya Kiserikali ikiwamo MCDI kupitia TFWG chini TNRF kampeni ilizinduliwa kwa majaribio. Hatua hii ya majiribio ilitekelezwa kwenye Wilaya mbili ambazo ni Kilwa na Rufiji

Kupitia majaribio ya utekelezaji wa kampeni jamii iliweza kujifunza mambo mbalimbali kama;

Hatua za uvunaji rasilimali za misitu ,Mbinu mbalimbali za kuboresha usimamizi shirikishi wa misitu Majukumu ya Serikali juu ya usimimazi na matumizi ya rasilimali za misitu.

Ø Thamani ya mazao ya misitu, Ø Jinsi ya kusimamia misitu

August 2012 Kampeni ilizinduliwa rasmi ngazi ya Taifa ikiwa na lengo kubwa la kuendeleza kuboresha utawala bora katika usimamizi wa misitu Tanzania pia kufanya kampeni katika Wilaya zingine zaidi ili kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu ili jamii iweze kunufaika na rasilimali hii ya misitu.

Malengo mengine;

Ø Kuiongezea jamii ufahamu juu ya haki ya umiliki wa misitu na ardhi

Ø Utekelezaji wa Sera na Sheria ya misitu

Ø Sheria ya ardhi

Ø Usimamizi wa wa biashara ya mazao ya msitu

Kampeni ya MM imefadhiliwa na;

Ø Ubalozi wa Norway

Ø Ubalozi wa Finland

Ø Kupitia Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF)

Kampeni hii itatekelezwa katika ngazi ya Kitaifa na ki Wilaya. Katika ngazi ya Taifa utekelezaji huu utafanya na mashirika kama Femina, LEAT, JET, TRAFFIC- TZ na TNRF-CCU

Katika ngazi ya Wilaya utekelezaji utafanywa kwa kupitia mashirika wadau kama ifuatavyo;

Ø MCDI- Kilwa & Nachingwea , Ø TFCG- Rufiji & Kibaha

Ø MJUMITA- Wilaya zote kupitia Mitandao yao, Ø WCST- Kisarawe

Katiaka kutekeleza shughuli za kampemi ya Mama Misitu katika wilaya ya Nachingwea vijiji vifuatavyo ndivyo vilichaguliwa kampeni hii kuanza kwao na jopo la uongozi wa wilaya. Vijiji hivi ni pamoja na:

Mbondo, Lionja B , Kiegei, Mbute , Namatumbusi, Mtua, Likwela, Ngangambo, Nyambi, Namatunu.

Vijiji vingine vitafikiwa na Kampeni hii kuanzia mwaka 2014

Katika utekelezaji wa kampeni hii, kazi hufanywa kwa ushirikiano wa wadau kutoka Nyanja tofauti tofauti. Baadhi ya wadau hao ni kama ifuatavyo;

  1. Halmashauri ya Wilaya Nachingwea

• Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira

• Taasisi za Usimamizi wa Sheria Wilayani hususan vyombo vya Usalama kama vile (Polisi, TAKUKURU, Mahakama, TRA)

• Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya

• Waheshimiwa Madiwani

• Vyombo vya habari

  1. Wanajamii katika Vijiji husika

• Halmashauri ya Kijiji

• Kamati za Maliasili

• Viongozi wa kata

• Mangariba/Wazee maarufu na vijana

• Vikundi vya sanaa

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top