BRANDTS AIONGOZA TIMU YAKE YA YANGA KUHANI MSIBA WA BABA WA NIZAR KHALFANI

clip_image001Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts (kushoto) pamoja na wenzake wakimpa pole Nizar Khalfan (kulia mwenye kofia). Nizar (kushoto) akisalimiana na Said Bahanuzi.…Haruna Niyonzima akimpa pole Nizar. Pembeni ni Jerry Tegete.Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa msibani.Nizar akiongea na kocha wake pamoja na alioambatana nao.Brandts akimuaga Nizar.

KOCHA Mkuu wa Yanga Ernie Brandts leo amekiongoza kikosi chake kufika nyumbani kwa kiungo wake Nizar Khalfan ambaye alifiwa na baba yake mzazi juzi jioni.

Nizar alifiwa na mzazi wake huyo aliyejulikana kwa jina la Khalfan Khalfan Jumamosi iliyopita baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimmbili ambako umauti ulimkuta.

Mara baada ya kutua nyumbani kwa Nizar kikosi hicho kikiwa na nyota mbalimbali walitoa mkono wa pole kwa Nizar pamoja na mdogo wake Razak Khalfan ambaye ni kiungo wa Coastal Union ya Tanga.

PICHA KWA HISANI YA GPL

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post