Unknown Unknown Author
Title: MALKIA WA NYUKI ABOMOLEWA JENGO LA OFISI YAKE, IKIWA NI UTEKELEZAJI WA AMRI YA MAGUFURI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rahma Al Kharusi, maarufu kama Malkia wa Nyuki. Na Saleh Ally UTEKELEZAJI wa amri ya Waziri wa Ujenzi na Miundombinu, John Pombe Magufuri,...

clip_image001Rahma Al Kharusi, maarufu kama Malkia wa Nyuki.

Na Saleh Ally

UTEKELEZAJI wa amri ya Waziri wa Ujenzi na Miundombinu, John Pombe Magufuri, umemuathiri Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharusi, maarufu kama Malkia wa Nyuki, baada ya moja ya ofisi zake jijini Dar es Salaam kubomolewa.

Ofisi hiyo ambayo ilikuwa inaendesha shughuli za kampuni ya kuuza mafuta ya RPB Oil inayomilikiwa na Malkia wa Nyuki, imebomolewa.

Bomoabomoa hiyo ya Magufuri imepamba moto katika Barabara ya Old Bagamoyo na majumba kadhaa yamebomolewa kwa kuwa kuna ujenzi wa kuitanua barabara hiyo.

Ofisi ya Malkia wa Nyuki ilikuwa katika ghorofa ya kwanza ya jengo la Green Acres, katikati ya makumbusho na Victoria na imevunjwa.

Ingawa jengo hilo halijavunjwa lote, lakini sehemu ya ofisi ya RPB Oil iliyokuwa upande wa barabarani imebomolewa yote.

Malkia ndiye mwanamama aliyetikisa katika soka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuilipia Simba zaidi ya Sh milioni 70 kwenda kuweka kambi nchini Oman.

Akalipa tena zaidi ya Sh milioni 50 kumpa kocha Milovan Cirkovic aliyekuwa anaidai Simba bila ya mafanikio. Baada ya hapo, Malkia amekuwa kimya na mashabiki wengi wamekuwa wakihoji kutaka kujua aliko.

Taarifa zinaeleza yuko nchini Oman anakoendelea na biashara zake, lakini ndugu yake mwingine alisema amebanwa na majukumu ya kampuni zake nchini Marekani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top