Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar .
Spika wa baraza la wakilishi Zanzibar Pandu ameir kificho amesema
Baraza la wakilishi liwe na Tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo
utekelezaji wake umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali
kuja kuingia katika kitahanani kwa lile ambalo kulitimizia Taifa
mahitaji yake muhimu.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la wakilishi wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura CCM Hamza Hassan Juma wakati alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nnje uzuuliwe kwani una uwasokosesha mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.
Amesema si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo kuzuia kuku kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wa
kutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.
“sivizuri kuzuia fungu hili na kukusema kuku wasiagiziwe kutoka nje bali tuwachie Serikali wakachunguze ukweli wa hilo na baadae watuleteeripoti,”alisema Spika.
Aidha ali sema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana
wananchi wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio
lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.
Nae waziri wa Nchi afisi ya Makamo wapili wa Rais Muhamed Abuod
Mohaamed alisema kuku wanao zalishwa na wanaanchi wa ndani ni tani 163 na nchi inahitaji tani 585 kwakujitosheleza kimahitaji ,hivyo
wazalishaji wa ndani bado uzalishaji wao mdogo.
Waziri huyo alilitaka baraza kua, wakiachie kifungu hicho na serikali
ya mapinduzi ya Zanzibar haina ajizi kuwapatia manufaa wananchi wake juu ya suala zima la uzalishaji kuku nchini, na wataliondoa pale
uzalishaji wa kutosha ukiwepo.
Ukiendelea mjadala huo waziri wa Afya Juma Duni alisema kumeingizwa kuku bandarini na kamapuni ya Malik Fereji ambao wamezuiliwa kutokana na mmiliki wa kuku hao kuidanganya Serikali kwa kutoa Risiti feki zisizo kuwa za kihalali ,kuibabaisha serikali juu ya kuku hao wanakotoka.
Wazri huyo ameseam kuku hao wazima lakini watangamizwa na mmiliki huyo atalazimika kulipia gharama za uangamizaji kutokana na kukosa uaminifu.
Nae mwakilishi aliokuwa amezuia kifungu hicho Hamza Hasssa Juma
alikubali kukiachia kifungu hicho kwa shingo upande kwa kuilaumu
serikali kua Bazara la Mapinduzi mapema washapitisha maamuzi
kuwasaidia wananchi kuinua zao la kuku lakini wahusika wake bado
wamelikalia kimya jambo ambalo halipendezi.
Alisema karibu duniani kote wazalishaji kuku katika nchi hupewa kipau
mbele kwa kupewa msukumo wa kifedha ili zao hilo kuzalisha kwa kiwango kikubwa kwa wazalendo na kulimiliki wenyewe wazalishaji wa ndani.
Aidha alisema haitowezekana kontena la futi 20 lililipiwa milioni 30
haponyuma na kwasasa kontena la futi 40 kulipiwa milioni nane
haiwezekani lazima ichnguzwe.
Mwakilishi aliishauri Serikali kumchukulia hatua za kisheria
muingizaji kuku kutoka kampuni ya Malik Fereji kwa kuidanganya
serikali kwa hati za ungo kuingizia kuku kutoka nchi sio.
“Inawezekana hata hao waliopita walingizwa kwa njia hiyo hiyo” alisema Hamza.
Hata hivyo alimuomba Spika ampe uhuru wa kuunda tume itayo weza
kujitegemea wenyewe kulifuatilia suala zima la kuku hapa Nchini na
Nnje ya Nchi kulifuatilia, na bila ajizi spika alikubali kuundatume
hiyo na kutakiwa kutafuta wezake wakufuatilia jambohilo.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.