Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI WA TARAFA YA PANDE WILAYA YA KILWA WALIA NA MBUNGE WAO KUTOHUDHULLIA VIKAO VYA BUNGE MARA KWA MARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katibu Mtendaji wa Asasi isiyo ya Kiserikali wilayani Kilwa, Omary Mkuwili akitoa maelezo mafupi kuhusiana na Mdahalo huo wa Uwajibikaji wa...
PANDE KILWA 001Katibu Mtendaji wa Asasi isiyo ya Kiserikali wilayani Kilwa, Omary Mkuwili akitoa maelezo mafupi kuhusiana na Mdahalo huo wa
Uwajibikaji wa Viongozi wa Serikali za Mitaa Chini ya Ufadhili wa The
Foundation na kufanyika jana katika Tarafa ya Pande wilayani Kilwa
PANDE KILWA 003Wadau mbalimbali waliohudhuria Mdahalo Huo
Na Abdulaziz Video,Kilwa
Wananchi wa kata ya Pande, wilayani Kilwa,mkoani Lindi wanakerwa na tabia ya mbunge wao wa Jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Bungala bwege ya kukwepa kushiriki kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri la muungano kwa muda Mwingi na hasa bunge la bajeti.

Wakizungumza kwenye mdahalo Unaohusu uwazi na uwajibikaji wa Viongozi na watendaji wa serikali za mitaa kwa maendeleo ya wananchi ulioandaliwa na Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilaya ya Kilwa, (KINGONET) kwa ufadhili wa The foundation for civil socitey na kufanyika katika shule ya Msingi ya Pande, wananchi hao, Akiwemo Bw Anan Nahoda, Saidi Athumani Kifuku na Mariamu Kajoka walisema kuwa muda wote wa kipindi cha mikutano ya bunge huko Dodoma mbunge huyo huwa anaonekana mitaani akifanya mikutano ya kuhamamsisha wananchi wagomee malipo ya pili ya korosho badala ya kuwa bungeni.
Anan Nahoda mkazi wa Pande alisema kuwa, kitendo cha Mbunge wao kukwepa vikao vya bunge vinawaumiza kwani moja kati ya kazi ya mbunge ni kuwakilisha mawazo ya wananchi kwenye mikutano ya bunge na kitendo cha mbunge wao kutokuwepo huko inaonyesha hatimizi wajibu wake ambao wapiga kura walimchagua hawatekelezewi.
Kinachotusikitisha sisi tuliomchagua ni kumwona mbunge wetu muda wote wa bunge yupo nje ya bunge tena kama kuondoka ni leo kwani hata jana alikuwepo hii inafanya tusiwe na mwakilishi kule bungeni hii si halali kwani hata akiwepo huku hashughuliki na masuala ya maendeleo
badala yake anaendesha mikutano ya ndani ya kushawishi wananchi wagomee malipo ya korosho”
alisema Anan.

Aidha Anan alilalamikia tabia ya mbunge huyo kutotembelea na
kutofanya mikutano na wananchi ili kukusanya kero na maoni
mbalimbali na kuyasemea akiwa bungeni na kudai kuwa tangu achaguliwa hajafanya mkutano wowote wa hadhara unaojumuhisha wananchi licha ya kufanya mikutano ya ndani.

Saidi Athuman alisema kuwa, tatizo la viongozi wengi waliochaguliwa
ni kutofahamu vyema mfumo wa vyama vingi kwani badala ya kushughulikia matatizo ya wananchi hujikuta wakishughulikia maslahi ya vyama vyao vilivyowawezesha kuwa madarakani hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kusababisha uvunjifu wa amani na kuwataka wajue majukumu yao kwa wananchi waliowachagua.

Kufuatia malalamiko hayo,Mtandao ulimtafuta Mbunge Huyo kwa njia ya Simu ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo Ambapo Bungala alikanusha tuhuma za kutofanya mikutano kwenye kijiji na kubainisha kuwa tangu amechaguliwa amefanya mikutano saba ambapo alikutana na wananchi mbalimbali kupokea kero zao na kuhusu la kutohudhuria bunge alikiri kutokwepa vikao vya bunge na kuwa hivi karibuni alionekana jimboni kwake na kudai kuwa alikuwa kwenye shughuli za uchaguzi mdogo ulizofanyika hivi karibuni wilayani Nachingwea ambapo alikwenda ili kusaidiana na viongozi wenzake kumnadi mgombea wa chama chake(CUF).
“Ni kweli sikuwepo kwani nilikuwa kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo huku Nachingwea ili kuhakikisha mgombea wetu anashinda na sasa hivi naelekea bungeni….hoja ya kutoonekana muda mwingi bungeni hiyo si kweli na ili la kutofanya mikutano si kweli labda huyo aliyelalamika hakuwepo…. kwani nimefanya mikutano mingi hapo na wa mwisho ni wa mwezi wa pili mwaka huu”alisema Bungala.

About Author

Advertisement

 
Top