Unknown Unknown Author
Title: WAMEANZA KUIJADILI NEMBO KUU YA TAIFA, TUNA KWENDA WAPI WATANZANIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Nembo ya Tanzania Nembo ya Tanzania ni ngao ya askari inayoshikwa na watu wawili. Ngao ina sehemu nne: juu sehemu ya dhahabu, chini yake ...

clip_image001

Nembo ya Tanzania
Nembo ya Tanzania ni ngao ya askari inayoshikwa na watu wawili.
Ngao ina sehemu nne: juu sehemu ya dhahabu, chini yake bendera ya taifa, halafu sehemu nyekundu na chini kabisa sehemu ya buluu-nyeupe
a) robo ya juu inaonyesha mwenge wa uhuru juu ya rangi ya dhahabu inayokumbusha juu ya utajiri wa madini ya taifa
b) robo ya pili ni bendera ya Tanzania
c) rangi nyekundu inamaanisha ardhi nyekundu ya Afrika na kilimo kama msingi wa maisha ya watu.
d) milia ya buluu na nyeupe katika robo ya nne inamaanisha mawimbi ya bahari na maziwa kwenye mipaka ya nchi pamoja na bahari inayozunguka Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Maungano.
Juu ya sehemu hizi kuna mkuki na majembe mawili yanayokumbusha juu ya utetezi wa uhuru na umuhimu wa kazi katika ujenzi wa taifa.
Ngao yote imeviringishwa na mapembe ya ndovu yanayomaanisha utajiri wa wanyamapori na hifadhi za taifa.
Ngao inalala juu ya mlima Kilimanjaro ambayo ni mlima mkubwa wa Tanzania.
Watu wawili wanaoshika ni mwanamume na mwanamke kama dalili ya ushirikiano wa jinsia zote mbili taifani. Wanasimama juu ya mpamba na mkarafuu ambayo yote inazaa mazao muhimu ya kibiashara ya Tanzania Bara kwa pamba na Zanzibar kwa karafuu.
Kanda njano ya maandishi chini ya ngao huonyesha wito la taifa “Uhuru na Umoja”
601944_533108306753168_1905714898_n

Tusipo kuwa waangalifu katika hili mgawanyiko utashamiri katika jamii zetu, Rai tuungane kama Miaka ya 60 kulinda amani na utulivu wa nchi yetu.

SOURCE: JF

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top