Unknown Unknown Author
Title: UPDATES ZA BREAKING NEWS: HAIJATHIBITISHWA KUWA SAIDA KAROLI AMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ZIWA VICTORIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Saida Karoli Mwanamuziki Saida Karoli anahofiwa kuwa amefariki  baada ya kuzama kwenye maji (drowning) kufuatia boti inayohisiwa kuwa m...
clip_image001
Saida Karoli
Mwanamuziki Saida Karoli anahofiwa kuwa amefariki  baada ya kuzama kwenye maji (drowning) kufuatia boti inayohisiwa kuwa mmoja wa abiria akisafiri nayo toka Kisiwa cha Goziba kuzama baada ya kukumbwa na dhoruba na kuzama Ziwa Victoria.
Inaalifiwa pamoja naye kuna watu wengine wamefariki dunia. mtandao wa wavuti.com umeripoti yakuwa:   

 Leo kumekuwepo na taarifa kutoka kwa mwanahabari, Frederick Katulanda kupitia kundi pepe la majadiliano la MabadilikoTanzania, zikiipoti kuwa mwanamuziki aliyekuwa maarufu Tanzania na Afrika Mashariki, Saida Karoli, amefariki dunia leo hii katika ajali ya kuzama kwa boti.

Kwamba, boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka katika kisiwa cha Goziba ilikumbwa na dhoruba ndani ya maji ya ziwa Nyanza (Victoria) na kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo na watu wengine waliokuwa wakisafiri pamoja katika chombo hicho.

Taarifa ya Neville Meena imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam na hajafariki dunia kama inavyoelezwa: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli... kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.” ameandika Meena.

Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “...ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria.”
 

SOURCE: WAVUTI.COM

About Author

Advertisement

 
Top