TAZAMA PICHA ZA LORI AINA YA SCANIA LILIVYOTEKETEA KWA MOTO JANA USIKU MAENEO YA MBEZI.

clip_image003Ajali hii ilihisisha gari aina ya SCANIA iliyowaka moto maeneo ya Mbezi Beach Samaki Chanzo cha ajali ni kulika sana kwa break na tairi ya upande wa kushoto kupata pancha hivyo kupelekea moto kuanzia hapo hapo kwenye tairi hilo na dereva kuona hivyo yeye na konda wake wakaruka kutoka nje kupitia dirishani na vile gari haikuwa na fire extinguisher so gari ikazidi kushika moto mpaka pale majira ya saa tatu kasorobo fire ya jiji la dar ilipofika na kujaribu kuokoa tanki la mafuta na tela la gari hiyo lisiendelee kushika moto na kusababisha mlipuko ambao ungeweza kutokea...

hakuna alieumia wala kujeruhiwa wala dereva hakukimbia alikua eneo la tukio kuanzia mwanzo hadi mwisho

HABARI NA PICHA NI KWA HISANI YA

Ammar Ruweih Nassor

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post