Taifa Stars imewasili leo hapa Marrakech, Morocco tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia ilifikia timu ya Ivory Coast ilipokuja kucheza na Morocco. Stars imetua na kikosi cha wachezaji 21 wakati Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu watawasili kesho- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana wakitokea Maputo, Msumbiji ambapo jana- Juni 2 mwaka huu timu yao ya TP Mazembe ilicheza mechi ya Kombe la Shirikisho.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 5 usiku.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.