Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imesema kuwa haiwezi kuziruhusu timu za Tanzania kushiriki katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati kutokana na hali ya usalama ya Darfur.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Amos Makalla baada ya gazeti hili kutaka kujua hatima ya timu za ushiriki wa timu za Tanzania katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
“Nipo kwenye kikao cha baraza la mawaziri, hata hivyo hatuwezi kuziruhusu timu zetu kwenda eneo ambao si salama, pamoja na kusubiri taarifa rasmi kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,” alisema Makalla.
Kauli hiyo inaifanya timu za Yanga kupoteza ubingwa wake, huku Simba na Super Falcon kuachana na mashindano hayo kutokana na sababu hiyo muhimu. Timu hizo pamoja na Shirikisho la Soka nchini, TFF lilikuwa linasubiri taarifa rasmi kutoka serikalini.
Awali, Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini, TFF, Leodegar Tenga alisema kuwa wao hawana taarifa zozote kuhusiana na uamuzi wa Serikali zaidi ya kauli yao ya kwanza.
“Sina taarifa, labda wewe una taarifa rasmi kuhusiana na uamuzi wowote kuhusiana na hatima ya timu za Tanzania katika mashindano hayo,” alisema Tenga ambaye pia ni Rais wa Cecafa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alisema kuwa hali ya usalama wa Darfur si nzuri na kuiomba TFF ifikirie upya uamuzi wa upeleka timu Darfur kwani kuna ushahidi kuwa hali ya usalama si nzuri.
“Tuna ushahidi kuwa hali ya Darfur siyo nzuri kiusalama, tumewaandikia TFF kuwaeleza hayo na kuwaomba wafikirie upya ushiriki wa Tanzania katika mashindano hayo,” alisema Membe.
SOURCE: MWANANCHI.COM
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.