SERIKALI ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imekumbwa na mpasuko baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kulalamika kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, hamtii bosi wake Rais Ali Mohamed Shein kufanya ndoa ya vyama hivi viwili CCM na CUF kukaribia kufika mwisho.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ametangaza kushirikiana na Rais mstaafu wa Awamu ya Sita Zanzibar, Dk Amani Abeid Karume ambaye atajiunga na chama cha CUF hivi karibuni kuhakikisha Zanzibar inapata mamlaka yake kamili haraka iwezekananvyo, "mimi ndiye Maalim Seif, nishazoea kufungwa, kutukanwa, kunyanyaswa hivyo hakuna ninalolihofia katika kuipigania Zanzibar" alisema huku akishangiliwa na wananchi na maelefu ya wanachama wa CUF katika viwanja vya Kibandamaiti.
“Madai haya si ya Seif, Karume, Jussa, Moyo au Eddy, ni sauti ya Wazanzibari wote kwanini tusiwe na mamlaka yetu kamili, kudai haki ni wajibu uliohimizwa na Mungu hivyo hatutakatishwa tamaa,”alisema Maalim Seif, alisema kabla ya kukatwa kwa mipaka na wakoloni mwaka 1884/1885 huko Berlin, Zanzibar ilikuwa ni Taifa kamili lakini baada ya kukatwa kwa mipaka hiyo ikabakishiwa visiwa vya Pemba na Unguja pamoja na maili kumi katika masafa ya usawa wa mwambao wa Pwani.
Amewahakikishia wananchi kuwa hatorudi nyuma katika kuitetea Zanzibar kuwa na mamlaka yake, ili iweze kutambulika kimataifa na kuweza kuratibu na kushughulikia mambo yake ya nje, tunataka kiti chetu UN, kiti chetu AU, tunataka sarafu, benki kuu, bendera yetu, vyama vya siasa vya kizanzabar na siyo kimuungano, baraza la mitihani pamoja na mafuta na gesi.
“vyovyote na iwe lakini Zanzibari ibaki huru yenye mamlaka yake kamili” kuanzia Jumatatu kila mzanzibar afike katika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti. Uwanja wa Kibanda Maiti utageuka “Tahrir Square” ya Misri na kuudhihirishia ulimwengu kwamba wazanzibari kwa amani kabisa wanataka mamlaka kamili ya nchi yao tukufu. Unamuogopa nani ewe mzanzibari? Ogopa nchi yako kuendelea kuwa chini ya ukoloni. Hapa ni Zanzibar kwanza, itikadi ni baadae. Viongozi mbali mbali wa vyama mbali mbali wazalendo wenye uchungu na nchi yao wanatarajiwa kuhudhuria alisema seif kuwa himiza wazanzibar wote wajitokeze kwa wingi.
Naye Mzee mmoja wa mjini Zanzibar ndugu Iddrissa Bin Al-Jumaa alisema hayote yanayoendelea ni wivu wa madaraka, unajuwa kijana wangu mwandishi, maalimu Seif anachuki na rais wa mapinduzi zanzibar Dr shein kwa kuwa Rais wa kwanza kutoka pemba...... hii inamuuzi sana Maalim Seif alitamani awe yeye, na kuhusu Dr Karume alisema yeye anachuki na viongozi wa bara kwa sababu walimuondoa kwenye urais, yeye Dr karume alitaka kujiongezea Muhura wa wa tatu lakini viongozi wa bara walimgomea na kumuweka Dr Shein, kuanzia hapo Dr Karume anachuki sana na serikali hii na ile ya muungano ndiyo maana anajiunga na maalimu seif sasa kuona Zanzibar inakuwa dola kamiri yenye mamlaka yake.
Source: Maisha Dunia Ngumu Jr
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.