Unknown Unknown Author
Title: OBAMA AKWAA KISIKI AFRIKA YA KUSINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waandamanaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Af...

clip_image001Waandamanaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya jana Juni 28

Afrika Kusini
WAKATI Rais wa Marekani Barack Obama akianza ziara yake nchini Afrika Kusini,baada ya kutoka Senegal kabla ya kufika nchini Tanzania,wananchi wa Afrika Kusini jana walimpokea Rais huyo kwa maandamano na mabango.
Maandamano hayo ya amani yaliandaliwa na kikundi cha waumini wa dini ya Kiislamu nchini humo na kuishia katika ofisi za Ubaloziwa Marekani, mada kubwa katika mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao ni kuhusu mauaji na vita vilivyo endeshwa na Marekani katika baadhi ya nchi za Kiislamu.
Waandamani hao walidai kwamba, Rais Obama na nchi yake ndiyo vinara wa vita nchini Iraq,Vietinam na baadhi ya nchi zingie za Kiislamu ambazo walidai kwamba ziliingia vitani kwa sababu za propaganda za Marekani.
Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika  jana Jioni - Juni 28
Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo jana  wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ..
Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu alibeba bango hilo jana  Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.

Picha Zote na REUTERS/AFP

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top