Mmoja wa waasisi wa Tanzania African National Union (TANU) na Chama cha Mapinduzi (CCM), Bi Halima Selengia maarufu kama 'Shangazi' (pichani) amefariki dunia leo mchana Moshi mjini nyumbani kwake Mtaa wa Liwali. Amefariki akiwa usingizini. Marehemu ambaye alikuwa na miaka 94 ameacha watoto wawili, wajukuu na vijukuu.
Msiba huu uko nyumbani kwa marehemu na kwa mujibu wa Familia ya Selengia, mazishi yamepangwa kufanyika kesho baada ya Salaat Jumaa kwenye makaburi ya waislam moshi mjini karibu na kuelekea na bohari ya BP.
Marehemu ni mmoja wa wazee waasisi wa chama cha TANU waliopambana bega kwa bega katika harakati za Uhuru. Amekuwa kiongozi wa akina mama wa Moshi mjini kwa muda mrefu hususan kuwa Mwenyekiti katika kuendesha mgahawa maarufu pale stendi ya moshi ujulikanayo kama Shangazi Mgahawa.
Wakati wa harakati wa uhuru mwaka 1956-57 Mwalimu Julius Nyerere alifikia nyumbani kwake katika harakati za kudai uhuru..
SOURCE: ISSAMICHUZI BLOG
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.