MJUE BONDIA WA KIKE MWAFRIKA “BINTOU YAWA SCHMILL” WA UJERUMANI

bondia

Unapozungumzia mchezo wa ngumi au ndondi nchini ujerumani Jina la Bondia wa kike mwafrika Bintou Yawa Schmill a.k.a "The Voice" ndiye anayemudu uringo "Boxing Ring" na kulipeperusha bara la Afrika ughaibuni.

Bondia huyo kike Bintou Yawa Schmill mwenye maskani kule Drackenburg nje kidogo ya mji wa Bremen,amekuwa kivutio kwa washabiki wa kimataifa na tishio kwa wapinzani wake anapokuwapo ulingoni.female prof.boxer Bintou Yawa SchmillBoxer Bintou Yawa Schmill mzaliwa wa Togo mwenye makao yake nchini ujerumani alianza kucheza ngumi akiwa na umri mdogo na kushinda mara 14 katika mashindano 24 na mara 4 K.O ,katoka draw mara 2 uzito wa Water weight 63.5 Kg, katika ngumi za ridhaa.

Kuanzia mwaka 2007 Boxer Bintou Yawa Schmill a.k.a "The Voice" alihamua kucheza ngumi za kulipwa kwa uzito wa Water weight 64.0 Kg, na urefu wa mita 1.70 , amepigana na kushinda professional Record 4 na Ushindi wa K.O mara 3.

Boxer Bintou Schmill kwa sasa kajiandaa kupambambana na bondia yeyote yule wa kike na mahala popote duniani.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post