MAN UTD, MAN CITY, ZA SAJILI LIVERPOOL YAFANYA VIPIMO NA ASPAS

clip_image001Guillermo Varela kutoka Uruguay amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa chini ya utawala wa kocha mpya wa Manchester United.Jesus Navas ametambulishwa leo na City baada ya kukamilisha uhamisho wa paundi millioni 14.5 kutoka Sevilla. Mchezaji huyu anakuwa wa pili kusajiliwa na Man City baada ya mbrazil FernandinhoIago Aspas anategemewa kukamilisha uhamisho wake kwenda Liverpool utakaogharimu kiasi cha £7.5million kutokea Celta Vigo baada ya leo mchana kuonekana akiwa nchini Uingereza tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya.

Aspas, 25, ambaye aliwasili England jana jumatatu, aliiambia Marca.com: "Nililazimika kukatisha mapumziko yangu huko Caribbean, ili kwenda England kukamilisha vipimo vya afya na Liverpool." Aspas anatajwa kuja kuziba pengo la Luis Suarez ambaye ametamka wazi kwamba anataka kuondoka huku akitoa ishara kwamba anataka kwenda Real Madrid baada ya leo kukaririwa akisema kwamba angependa kucheza timu moja na Cristiano Ronaldo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post