LIONEL MESSI NA BABA YAKE WATUHUMIWA KUKWEPA KULIPA KODI YA PAUNDI MILLIONI 3.4

clip_image002Mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi ametuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha  £3.4million.
Mashataka yamefunguliwa dhidi ya mshambuliaji huyo wa Barcelona na baba yake mwendesha mashtaka wa kaskazini mashariki mwa Catalunya, mahala ambapo Messi anaishi.
Wote wawili Messi na, Jorge Horacio, wanatuhumiwa kwa makosa matatu dhidi yao kwa kudanganya taarifa juu ya ulipaji kodi ambayo inafikia kiasi cha £3.4m cha kodi ya mapato katika miaka ya 2007, 2008 na 2009.
Jaji katika mahakama inabidi ayakubali mashtaka ya mwendesha mashtaka kabla ya kesi kufunguliwa rasmi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post