TIMU YA TAIFA YA TANZANIA (TAIFA STARS)
NA FUNDI SAYORE
Ukweli ni kuwa, kwa Group C. hakuna atakayemzuia Ivory Coast kwenda Round 3 (Play-offs round). Inabidi tuwe wakweli; wao ndio timu imara, wana consistent na muhimu zaidi wana uzoefu mkubwa kwenye letu. Hata hapa Dar, tutapata taabu kupata droo au ushindi. That's how good they are.
Ila mimi mtazamo wangu tofauti, we are still suffering the '1994' Syndrome. Mnaijua ni nini?
Kati ya mwaka 1992-1995, tuliwahi kupata 'The Golden Generation of Tanzania Football' never to have qualified for the major tournament. Tanzania tulikuwa tunatawala michuano ya CECAFA. Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (sasa Kagame Cup) lilikuwa likibadilisha vilabu vya hapa from Simba to Yanga na hata Mlandege.
Bara walibeba Challenge mwaka 1994, Zanzibar 1995, Simba ilifika fainali ya Kombe la CAF 1993 huku Malindi ikifika nusu fainali ya Kombe hilo hilo mwaka 1995. Semi-professional ilikuwa ndiyo imeingia kwenye soka letu, na kwa bahati nzuri tulikuwa na wachezaji waliopokea mfumo huo.
Lakini tulikosa kitu kimoja, ushiriki wa Kombe la Mataifa Afrika na Kombe la Dunia. The previous tournament (1994 Tunisia) Tanzania na Liberia tulijitoa kwenye hatua za awali kutokana na ukata pamoja na machafuko Liberia. Lakini kuelekea 1996 (wakati huo AFCON ikiwa inatarajiwa kufanyika Kenya kabla ya maandalizi kuwashinda na kuhamishiwa South Africa), Taifa Stars waliamua kushiriki na kupangwa Kundi gumu la timu 6 lililokuwa na vigogo kama Misri, Algeria, na wana CECAFA wenzetu Uganda, Sudan na Ethiopia. Kundi hilo lilitakiwa kutoa timu mbili kuelekea AFCON baada ya michezo 10.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya sasa ya saidia Stars ishinde
Stars ikiundwa na wachezaji wengi wa Simba walioipeleka Simba fainali ya CAF mwaka 1993 pamoja na baadhi wa Yanga, Small Simba na Malindi, walianza mechi ya kwanza Kirumba Stadium na kukutana na Uganda Cranes (kipindi hicho ikiwa na nyota kama Majjid Musisi (RIP), Jackson Mayanja' Lunyamila', Paul Hasule (RIP), George Ssemogerere, Adam Semugabi, Sule Kato etc). Stars ilikuwa chini ya kocha Sunday Kayuni aliyetengeneza jina lake kupitia Sigara (kama sikosei) ya DSM. Nakumbuka Stars iliwachabanga waganda mabao 4-0 huku Lunyamila akitupia mabao mawili pamoja na jingine kutoka kwa Nteze John. Perfomance ya Stars ikiongozwa Lunyamila ilikuwa juu mno na expectations za watanzania (kama kawaida yetu) zikapanda juu balaa.
Then tukarudishwa kwenye ukweli mechi iliyofuatia baada ya kufungwa mabao 5-1 na mafarao kabla ya kurudi nyumbani na kuwatandika Sudan mabao 2-0 (Mzee wa Kiminyio akitupia mabao yote) uwanja wa Taifa.
Sasa issue ilikuja pale tulipowatandika Algeria mabao 2-1 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kimsimamo tulikuwa nafasi ya pili kwenye Group nyuma ya Misri na safari ya kuelekea South Afrika ikionekana nyeupe. Serikali ikaibuka ghafla na kuunda "Kamati ya Saidia Stars Ishinde" ikiongozwa na matajiri wenye pesa enzi hizo akiwemo Azim Dewji. Kazi ya kwanza (katikati ya tournament) ya kamati wakatafuta Kocha Mbrazil Oliveira, Kayuni akatupwa kando, wachezaji wakajazwa pesa balaa ili wasiwaze kingine zaidi ya soka. Tukaanza maandalizi katikati ya mashindano.
Kilichofuatia yalikuwa majanga. Tulimaliza vibaya balaa. Tulishinda mechi moja kati ya 5 zilizofuatia na zilizobakia zote tukafungwa. Stars ikamaliza ya 4 kwenye kundi lake huku Misri na Algeria zikielekea South Africa.
Since then hatukujifunza na makosa yetu. Olivera aliondoka so was Dewji, Kayuni alielekea pande za Mtibwa (kama sikosei) and we never replaced that generation adequately mpaka wakati wa Marcio Maximo labda. Hatukuamka tuwe na Youth Programs, wala kuhakikisha serikali inahusika na maandalizi ya muda mrefu wakati mwingine. It never happened na tumekuwa tukirudia kosa lile lile tangu mwaka 1994, 'Kamati ya Saidia Stars Ishinde' katikati ya michuano.
So Morocco may be a start of the end. Kuna sababu nyingi dhidi yetu. i.e. Morocco wanataka sana kufanya comeback, wakati huu ni wa mapumziko kwenye lig za ulaya hivyo wapinzani wetu wana wachezaji wao wote.The Ivory Coast factor and above all starting pumping money into team at mid-tournament. Na sitashangaa 'The Elephants' wakichukua pointi 3 Dar na tukaangukia kwenye mikono ya Gambia na kufungwa. Who knows?! tumerudia makosa ya 1994 and we are paying for it.
Naipenda Taifa Stars, LAKINI TUBADILIKE.
FUNDI SAYORE
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.