Sakata la usajili wa mchezaji Cristiano Ronaldo limezidi kupamba moto - wakati taarifa kadhaa kutoka barani ulaya zikisema kwamba Ronaldo anatarajia kusaini mkataba mpya na Real Madrid huku wengine wakisema yupo njiani kurejea Manchester United - leo hii mapema mchana Cristiano Ronaldo alitumia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Twitter kukanusha taarifa zote zinahusu kuongeza mkataba wa kuichezea Real Madrid. Hata hivyo Ronaldo ameendelea kukaa kimya kuhusu taarifa za kutaka kurejea United.
Kwa wiki kadhaa taarifa za kurudi Man United kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 65 zimekuwa zikisambaa huku Raisi wa Madrid Florentino Perez akisisitiza anataka kumbakisha Cristiano kwa gharama yoyote.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.