Boti mpya ya kisasa ya Azam Marine, Kilimanjaro IV ikiwa imeshushwa katika bahari ya Hindi eneo la Zanzibar mchana wa leo tayari kuanza kazi kwa safari za Dar es Salaam na Zanzibar.
Mmiliki wa Makampuni ya S.S. Bakhresa, Alhaj Said Salim Awadh Bakhresa (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Maji Zanzibar (ZMA) na kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa kampuni yake, Jaffar Iddi
Kilimanjaro IV kabla ya kushushwa kwenye Meli iliyoileta nchini
Inashushwa...
Inateremshwa majini
Azam Marine wamekarabati pia eneo la abiria kupumzika wakisubiri usafiri na mfumo mzima wa huduma hadi ofisi za kisasa
Ofisi mpya za Idara ya Uhamiaji Azam Marine
Ofisi mpya ya Polisi
Abiria wanastarehe sasa
Burudani kwenye Luninga kubwa wakati unangoja boti
Meneja Mkuu wa Azam Marine, Omar Mohamed Said kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Kilimanjaro IV
Mzee Bakhresa alikuwa bize mpaka basi leo
Anatazama Meli inavyoshushwa
Mwonekano wa Nje unapoelekea kupanda boti za Azam Marine
Namna hiyo, kila kitu kinakwenda sawa
Mzee Bakhresa pembeni ya Abdulrazak, moja kati ya majembe ya Azam Marine
Baaas, iwekeni hapo hapo na mtie nanga; Mzee Bakhresa akitoa maelekezo
Tags
HABARI ZA KITAIFA