Unknown Unknown Author
Title: Live Match: Harambee Stars itawang'oa mabawa Eagles?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hii leo Kenya inajiandaa kushuhudia mchuano wa kufa kupona kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katik...
clip_image001Hii leo Kenya inajiandaa kushuhudia mchuano wa kufa kupona kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani mjini Nairobi kuanzia saa kumi jioni saa za Afrika Mashariki.
Hii ni mechi ya mkondo wa pili kwa timu hizo mbili baada ya kwenda sare ya bao moja kwa moja walipocheza kwa mkondo wa kwanza mjini Calabar Nigeria mwezi jana.
Mechi hii ni ya kundi la F ya kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Vijana wa kocha Stephen Keshi, wanatarajiwa kuendeleza ushindi wao hii leo wakijitafutia nafasi ya kuwakilisha Afrika katika michauno ya kombe la dunia nchini Brazil
Kwa vijana wa Eagles wanaosemekana kujiandaa vyema, wanafahamu kuwa ikiwa watashindwa basi itakuwa hasara kwao kwani hawataweza kwenda Brazil.
Licha ya kwenda sare mwezi jana, Nigeria inaingia kwenye mkondo huu bila ya kushindwa mechi yoyote ya makundi kati ya kumi na sita zilizocheza hadi kufikia sasa.
Wadadisi wanasema Eagles wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda. Mwandishi wetu Odeo Sirari amepiga kambi katika uwanja wa Moi Kasarani kutupasha habari. Na wewe shabiki una fursa ya kutupasha yanayojiri huko pia kupitia kwa ukurasa wtu wa Bofya facebookBofya bbcswahili


14:50 PM :Shamra shamra zimeanza kupamba moto katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani. Mwandishi wa BBC ambaye yuko katika uwanja huo Odeo Sirari, anasema kuw mashabiki wanzidi kumiminika uwanjani. Milango ya uwanja ilifunguliwa rasmi majira ya saa tano asubuhi
14:58 PM: Mojawapo ya mabango ya mashabiki uwanjani yana bendera ya Kenya na maandishi ''Oga you are finished'' kwa maana kuwa Nigeria itashindwa . Odeo anasema hayo ni maoni ya mashabiki wa Nigeria uwanjani

Timu zote zina mbili zina uhakika zitashinda mechi ya leo. Tuache tuone msema kweli
Mechi inatarajiwa kuanza saa kumi kamili. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria


15:43 PM: Mashabiki washangilia wachezaji wa Harambe Starrs wakiingia uwanjani. Super Eagles nao pia wameingia uwanjani . Wachezaji wa pande zote mbili sasa wanapasha misuli joto
15:48 PM: Uwanja wa michezo wa Moi Kasarani una uwezo wa kushenei mashabiki takriban 60,000
15:49 PM: Kikosi cha Harambe Stars: Mlinda lango Duncan Ocheng, Safu ya ulinzi David Owino Brian Mandela David Ochieng . Wachezaji wa kiungo cha kati Mulinge Ndeto, Victor Wanyama Jamal Mohammed,Johana Omolo na Peter Opiyo. Washambulizi ni Kefa Aswani na Fracis Kahata


16:07 PM: Mechi imeng'oa nanga rasmi . Kikosi cha Eagles...Efe, Oboabona, Omeroo Elderson, Onazi, Mikel, Mba,Oduamadi,Musa, Ideye Golikipa ni Enyeama

16:33 PM baada ya mechi kuchezwa kwa zaidi ya dakika thelathini bado timu hizo ziko sare tasa

16:39 PM Humphrey W. Musungu kupitia ukurasa wetu wa Bofya facebook anasema David owino ajeruhiwa lakini anashughulikiwa

16:41 Mshambuliaji wa Kenya Kepha Aswani anenekana akichechema uwanjani na kuwa mashabiki wanataka aondolewe


16:51 shambulizi katika eneo la hatari lango la timu ya Kenya. Sunday Mba aliupiga mpira kwa kichwa lakini ukapaa juu ya mlingoti wa goli . Mashabiki wa Kenya wabaki kimya


17:27 pm Peter Opiyp atekeleza shambulizi lango la Nigeria.

17:28 Nigeria yafanya mabadiliko, SundayMba aondolewa

17:28 Victor Wanyama apata jeraha..anahudumiwa. Kenya yashambulia, Kombora la Johhana Ngeno lapaa juu ya mlingoti kunako dakika ya 56. Victor Wanyama arejea uwanjani, mashabiki wa kenya washangilia. Nigeria inahitaji ushindi katika mechi hii dhidi ya Kenya ili kusonga mbele. Sare ya kutofungana itaipa Kenya nafasi nzuri ya kusonga mbele

17:38 pm: Mlinzi wa kati wa Harambee Stars Brian Mandela afanya kazi ya ziada kupangua makombora ya wa Nigeria.

Mashabiki wa Kenya wanaimba: '' Haki yetu! Bao! Haki yetu! bao!

Victor wanyama aondoka tena uwanjani, yamkini jeraha lake ni baya.

Timu ya taifa ya Nigeria yafanya mabadiliko dakika ya 64 anaondoka Brown Aye anaingia Ujah Antony

17:39 pm: Victor Wanyama arejea tena uwanjani licha ya kuonekana amejeruhiwa. Mashabiki wa Kenya wanataka aendelee kucheza.

17:40 Mulinge Munandi aonyeshwe kadi ya njano kwa kumfanyia masihara mchezaji wa Nigeria Musa Ahmed. Harambee stars yazidisha shinikizo dhidi ya Super Eagles. Mashabiki wakosa subira.. wanaimba haki yetu! bao! haki yetu! bao.....

Peter Opiyo wa harambee stars aondolewa, Patrick Osiako aingia uwanjani.


17:52 pm: Mashabiki wa timu ya taifa ya Nigeria kama mia 200 hivi washangilia bao lililofungwa na Musa Ahmed. Baadhi ya mashabiki wa Kenya wawazomea wenzao wa Nigeria kwa kuwarushia chupa za maji.

Safu ya mashambulizi ya Harambee stars yaonekana kufifia.

Dakika ya 87, Oduamani wa Nigeria aondoka anaingia Ogude.

Nigeria yapata kona ya pili kipindi cha lala salama.

About Author

Advertisement

 
Top