Unknown Unknown Author
Title: HANS POPPE AVAMIA TUNISIA KUDAI FEDHA ZA OKWI, ASEMA ANAKWENDA KULIANZISHA KWELI TENA ILE KINOMANOMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe anaondoka kesho Morocco, kwenda Tunis, Tunisia kufuatilia fedha za mauzo za...

clip_image001MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe anaondoka kesho Morocco, kwenda Tunis, Tunisia kufuatilia fedha za mauzo za aliyekuwa mshambuliaji wa klabu yake, Mganda Emanuel Anord Okwi dola za Kimarekani, 300,000.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY mjini hapa, Poppe alisema kwamba amelazimika kwenda huko baada ya kuona klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia inapiga danadana kulipa deni hilo.
Poppe alisema ataungana na Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala ambaye tayari yuko Tunis kwa ajili ya kupambana na Etoile kupata fedha zao.
“Tumekuwa tukiwaandikia sana barua Etoile lakini hawajibu, sasa tumeamua kufuata kanuni, tunaanzia kwenda kushitaki kwenye FA yao, baada ya hapo tunakwenda FIFA,”alisema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Okwi aliuzwa katika klabu hiyo Januari mwaka huu na hadi sasa Simba SC imekuwa ikisotea fedha za muazo yake.  
Poppe alikuwa hapa kuisapoti timu ya taifa, Taifa Stars ambayo jana ilicheza na wenyeji Morocco katika mchezo wa Kundi C, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Stars ilifungwa 2-1 Uwanja wa Marakech jana na sasa iko tayari Uwanja wa Ndege wa Mohamed V, Casablanca kurejea Dar es Salaam ikipitia Cairo, Misri na wiki ijayo itacheza mechi nyingine ya Kundi dhidi ya Ivory Coast nyumbani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top