Unknown Unknown Author
Title: EURO U-21: SPAIN MABINGWA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
NAHODHA wa Kikosi cha Spain cha Vijana chini ya Miaka 21, Thiago Alcantara, alipiga Hetitriki katika Kipindi cha Kwanza walipoifunga Italy...
clip_image001
NAHODHA wa Kikosi cha Spain cha Vijana chini ya Miaka 21, Thiago Alcantara, alipiga Hetitriki katika Kipindi cha Kwanza walipoifunga Italy Bao 4-2 katika Fainali ya EURO U-21 na kutwaa Ubingwa wao wa nne.
Thiago alitangulia kuipatia Bao Spain na Italy wakasawazisha kwa Bao la Ciro Immobile kufuatia pasi ndefu ya Giulio Donati.
Lakini Thiago akaipa tena Spain Bao la kuongoza na pia kupiga Bao la 3 kwa Penati.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 3-1.
Kipindi cha Pili Isco akaifungia Spain Bao la 4 kwa Penati na Fabio Borini kuipatia Italy Bao la pili. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Spain kutwaa Ubingwa wa Ulaya wa U-21 na ni mara ya 4 kwa wao kutwaa Ubingwa huo.
JE WAJUA?

MTOTO wa Mchezaji wa zamani wa Klabu za US Lecce na ACF Fiorentina, Mazinho, ambae alitwaa Kombe la Dunia Mwaka 1994 akiwa na Brazil, ndie Nahodha wa Spain U-21 Thiago Alcántara ambae alizaliwa Kusini mwa Italy???


VIKOSI:

ITALY U21:

01 Bardi, 02 Donati, 06 Caldirola, 13 Bianchetti, 19 Regini, 04 Verratti, 07 Florenzi, 21 Rossi, 09 Immobile, 10 Insigne, 20 Borini

Akiba:

12 Colombi, 22 Leali, 03 Biraghi, 05 Capuano, 08 Marrone, 15 Sansone, 16 Bertolacci, 18 Saponara, 23 Crimi, 11 Gabbiadini, 14 Destro, 17 Paloschi

SPAIN U21:

01 De Gea,  02 Montoya, 05 Bartra,  06 Martinez, 18 Moreno, 03 Illarramendi, 08 Koke, 10 Thiago, 11 Tello, 12 Morata, 22 Isco

Akiba:

13 Marino, 23 Robles, 04 Nacho, 15 Muniesa, 16 Gonzalez, 20 Carvajal, 14 Camacho, 17 Sarabia, 09 Moreno, 19 Muniain, 21 Vazquez

ANGALIA HIGHLIGHT YA MECHI HIYO HAPA

About Author

Advertisement

 
Top