Tukio la bomu la Arusha limewasitua wengi kufuatia vifo vya wananchi wanne wasio na hatia....
Nasema hawana hatia kwa sababu siku ya tukio wananchi hao walikuwa katika mkutano wa hadhara wa chama chao ( CHADEMA ) sawa na ambavyo wangeweza kuwa katika mkutano mwingine wowote wa kisiasa....
Pamoja na majonzi waliyonayo wananchi, wanasiasa wetu wanaonekana kutoguswa kabisa na vifo hivyo ambavyo kwa mtazamo wangu nathubutu kusema kuwa chanzo cha yote ni wao .....
Jana kupitia account yake ya twitter, mbunge Serukamba alidai kuwa tukio la Arusha halimpi fundisho lolote zaidi ya fundisho moja tu kwamba TANZANIA KUNA WANARIADHA WAZURI.....
Tunapata fundisho gani hapa???... Ndugu zetu wamekuwa wakipoteza maisha kila mara kupitia mikutano ya wanasiasa wetu....
Cha kushangaza ni kwamba, wanasiasa haohao wamekuwa wakitucheka na kutudhihaki...!!!
Kauli hii ni fundisho tosha.
Najaribu kuihusisha kauli ya mbuge huyu na tusi la nguoni alilowahi kulitoa bungeni la "COME ON FU**K U"...ili nimjue alivyo
Matukio haya yanatosha kumpima Serukamba na kumjua jinsi alivyo...!!!
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.