Unknown Unknown Author
Title: CANNAVARO NA SSENKOOM WALIVYO TOFAUTI, NANI ANAHAMIA?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jionee tofauti; Ssenkoom kulia akiwasili Dar es Salaam jana na Cannavaro kushoto akiondoka Dar es Salaam wiki iliyopita. Tazama mabegi yao, ...

clip_image002Jionee tofauti; Ssenkoom kulia akiwasili Dar es Salaam jana na Cannavaro kushoto akiondoka Dar es Salaam wiki iliyopita. Tazama mabegi yao, yupi anahamia, yupi anasafiri mara moja na kurudi.

Na Mahmoud Zubeiry,

KITU kimoja tu jana kilinifanya nikamuangalia mara mbili mbili beki mpya wa Simba SC, Samuel Ssenkoom baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kutokea kwao, Uganda kuja kuanza maisha mapya Msimbazi.

Alikuwa kama mtu ambaye amekuja na atageuza mara moja tu, hakuwa na mzigo mkubwa. Alikuwa na kabegi kadogo, ambako sana katakuwa na nguo za kubadilisha mara moja.
Nilitamani kumuuliza Ssenkoom juu ya hilo, lakini kuna mtu anaitwa Daniel Manembe, rafiki yake sana Nahodha wa Simba, Juma Kaseja alinizuia kuuliza maswali zaidi, akisema mchezaji anatakiwa akapumzike amechoka kwa ‘safari ndeefu’ ya saa zisizozidi tatu kutoka Kampala.

Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ndiye aliyempokea. Tazama hapa hajambebea chochote. Hicho kibegi cha nguo mbili ndio amekuja nacho Ssenkoom kuanza maisha mapya Msimbazi

Kwa hivyo nikabaki nawaza mambo mengi tu, labda amepanga kuja kununua vitu huku huku Dar es Salaam baada ya kupokea mlungula wake wa kusaini Mkataba wa miaka miwili.
Maana tumezoea hata wachezaji wetu wanaposafiri japo safari ya wiki moja tu kwenda kucheza mechi nje, mabegi yao huwa makubwa wastani na yameshiba.
Na mfumo wa maisha kwa wachezaji wote wanapokuwa ugenini hautofautiani, baada ya mazoezi wanarudi kambini kupumzika- hawana nafasi ya kwenda kuzurula.
Lakini kwa mchezaji ambaye anakwenda kuanza maisha mapya katika klabu, lazima atakapowasili atakuwa katika mwonekano wa mtu anayehamia.
Bado sijui, Ssenkoom atarudi Uganda baadaye kuongeza vifaa vyake- au atafanya shopping huku huku Dar es Salaam, maana unaweza kujionea tofauti hata katika picha zilizotumika hapa kati yake na beki wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wakati anasafiri na timu ya taifa, kwenda Morocco kwa kupitia Ethiopia.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top