BREAKING NEWS: SIMBA NA YANGA HATARINI KUSHIKIRI KOMBE LA KAGAME DARFUR

clip_image002Siku kadhaa baada ya Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati - CECAFA kuidhinisha michuano ya kombe la Kagame kuchezwa mjini Darfur -Sudan, serikali ya Tanzania imetoa tamko kuhusu timu za Simba na Yanga kwenda kushiriki michuano hiyo huko Sudan kwenye eneo ambalo limekuwa likiandamwa na vurugu kwa miaka kadhaa sasa.
Kwa mujibu wa msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga ni kwamba serikali haidhani ni busara kwa vilabu vya Simba na Yanga kwenda kwenye eneo hilo kushiriki Kagame Cup kutokana hali mbaya ya usalama iliyopo Darfur.
HIVI NDIVYO ALIVYOANDIKA KAMWAGA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK.
Ezekiel Kamwaga

Breaking News...... Serikali imesema haioni busara ya Kagame Cup kupigwa Darfur.... Hakuna hoteli ya maana na watu wanashauriwa kutembea na fulana zinazozuia risasi kupenya... Nadhani hii ndiyo stori kubwa ya kimichezo kwa leo.... Je, mnadhani itakuwa busara kwa Simba na Yanga kushiriki?

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post