Unknown Unknown Author
Title: BASKET BALL KITAA ALLSTAR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
B'BALL KITAA ALLSTAR KUWASHA MOTO JUMAPILI Ikiwa baada ya Kumpata Mshindi wa Mashindano ya Mpira wa Kikapu Maarufu kama B'BALL KIT...

clip_image002

B'BALL KITAA ALLSTAR KUWASHA MOTO JUMAPILI

Ikiwa baada ya Kumpata Mshindi wa Mashindano ya Mpira wa Kikapu Maarufu kama B'BALL KITAA kwenye fainali iliyofanyika jumapili Iliyo Pita kati ya EAST ZONE 4 na WEST ZONE 1,ambayo EAST ZONE 4 kuibuka bingwa,Mashindano hayo Yatafikia Kileleni Jumapili hii JUNE 23,2013 pale pale Viwanja vya Gymkhana Posta.

Katika Kuhitimisha Mashindano hayo kwa Mwaka huu,B'BALL kitaa Imeandaa GAME ya All star ambayo Itakuwa inashirikisha Wachezaji wakali kutoka west zone Watapambana na wakali wengine Kutoka EAST ZONE.Richa ya Mshindi wa Mashindano Kutoka EAST ZONE,wakali wa WEST ZONE wamejinadi na kusema Katika GAME ya ALLSTAR EAST ZONE itakuwa katika wakati Mgumu sana.Tayari Timu PANDE ZOTE Mbili zimeshaandaliwa na Wachezaji walionesha Kiwango cha Juu kutoka kila pande tayari majina yao yamewekwa hadharani na waandaji wa Mashindano Hayo kupitia Page yao Ya Facebook.Itakuwa ni Game Ngum u,yenye Vuta ni Kuvuta na Ushindani Mkubwa sana kutokana na Kila Kanda(zone) Kuonekana kuwa na Kikosi Kizuri sana.Inakuwa Ngumu kutabiri ni nani ataibuka Kifua Mbele kwenye Mashindano hayo kutokana na TIMU ZOTE Kuwa na wachezaji waliokuwa katika kiwango Kizuri sana.

WEST ZONE:Ukanda Huu unaoshirikisha Wachezaji Kutoka upande wa Magharibi wa Dar es salaam,utawakilishwa na wachezaji BORA 12 waliochaguliwa kutoka kwenye Timu za  WEST ZONE 1,2,3 Na 4.Hii itajumuisha wachezaji kutoka maeneo Ya MBEZI,KAWE,KUNDUCHI,TEGETA,MWENGE,SINZA,KNYAMA,UBUNGO,M/NYAMALA,KINONDONI,MAGOMENI,BUGURUNI,VINGUNGUTI NA UKONGA.Katika Ukanda Huu wachezaji waliochaguliwa kuunda Kikosi cha WATANO Wakuanza(FIRST FIVE STARTERS) Ni JOJO KISUSI,BARAKA MAPELE,SAJO SAMUEL,FRANK MWENEZI,CHACHA TUBET,,na wengine watakoa anzia Reserves Ni ABEL LINUS,STEVEN MACHO,CRISS ASUTO,MAIGE YUNZU,MAKANI MOHAMMED,ALLY MOHAMMED NA MKONGWE JUMA KISOKI.

WEST ZONE itakuwa chini ya KOCHA mzoefu na Maarufu sana Kwa Wapenzi wa Basketball Dar es Salaam/Tanzania COACH MOHAMMED MBWANA.

EAST ZONE:Ukanda Huu unaoshirikisha wachezaji Kutoka Upande wa Mashariki mwa Dar Es Salaam,Utawakilishwa na wachezaji BORA 12 waliochaguliwa kutoka kwenye Timu za EAST ZONE 1,2,3,4.Hii itajumuisha wachezaji kutoka maeneo Ya MIKOCHENI,KINO-MOROCCO,NAMANGA,OYSTERBAY,MASAKI,MSASANI,UPANGA,DOWN TOWN,KARIAKOO,ILALA,TEMEKE,TANDIKA,KURASINI NA MBAGALA.Katika Ukanda Huu wachezaji waliochaguliwa kuunda Kikosi cha WATANO Wakuanza(FIRST FIVE STARTERS)ni STEVEN MTEIONGA,ANDREW KUNGUA,SALIM MCHEMBA HUSSEIN,ZAHORA ZAHOR,MURSHID MUDRICAT huku na wengine watakoa anzia Reserves Ni ADAM GIGAME,EVANGE KAMOLA,SAIDI MABISI,MUSA CHACHA,MARTIN KOLIKOLI,MUSA NASSORO,NA MWALIMU KHERI

EAST ZONE itakuwa chini ya uangalizi wa Kocha WILLIAM MZIRAY maarufu kama COACH WILLY.

KWA WAPENZI WA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA hutakiwi kukosa kabisa kwani MECHI HIYO ITAYOJUMUISHA WAKALI HAO wa west zone na East Zone  ITASINDIKIZWA NA BURUDANI MBALI MBALI ZA MUSIC HASAA WA HIP HOP.kwa Habari zaidi Unaweza Kuwapenda(like) B'BALL kitaa kwenye page yao ya Facebook BBALL KITAA au Kuwafata(follow)kwenye  Account yao ya Twitter @BBALLKITAA.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top