Unknown Unknown Author
Title: RIHANA AMSHINDA JUSTIN BIEBER KWA VIDEO ZAKE KUTAZAMWA ZAIDI MTANDAONI, CHEKI WASANII WANAOONGOZA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Robin Rihanna Fenty a.k.a Rihanna anazidi kung’aa kwenye ulimwengu wa RnB mwaka huu, baada ya kuvunja record kwenye billboard charts sasa am...

clip_image001Robin Rihanna Fenty a.k.a Rihanna anazidi kung’aa kwenye ulimwengu wa RnB mwaka huu, baada ya kuvunja record kwenye billboard charts sasa amehamia kwenye vichupa vyake 77 vilivyo You Tube ambapo ameichukua nafasi ya kwanza kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi ya waimbaji wenzake na kumfunika Justin Bieber aliyekuwa ameishikilia nafasi hiyo.

Video za Rihanna zimefikisha jumla ya watazamaji billion 3.788 hadi kufikia jana jumanne(june 18) wakati Justin Bieber mwenye vichupa 79 vya kutazamwa amezidiwa na Rihanna watazamaji million 2.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na Mkorea ‘PSY’ mzee wa ‘Gangnam Style’ ambae amepata jumla ya watazamaji billion 3.1 wa video zake zote, nafasi ya nne imeenda kwa rapper asiyechuja Eminem mwenye jumla ya watazamaji billion 2.4, the mother monster ‘Lady Gaga’ amemfuata Eminem kwa kuwa na watazamaji billion 2.3, na nafasi ya tano imeenda kwa Ray C wa mtoni ambae kiuno chake hakiongopi ‘Shakira’ ambae amepata jumla ya watazamaji billion 2.

Kwa upande wa mtandao wa kijamii wa Twitter bado justin Bieber ndiye mfalme wa Twitter kwa kuwa na followers wengi zaidi ya wasanii wenzake. Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa msanii wa kwanza kwa walio hai kufikisha idadi ya followers million 40 na kumfunika mkongwe Lady Gaga.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top