BAADA YA VIFO VINGI, WASANII WAHAMASISHANA KUMRUDIA MUNGU

clip_image001

KUTOKANA na vifo vya mara kwa mara vya wasanii, staa wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameibuka na kusema ni wakati wa wasanii kumrudia Mungu.

Akizungumza na mwandishi  wetu hivi karibuni, Dude alisema kwa kipindi kifupi vimetokea vifo vingi vya wasanii tena wenye umri mdogo, hivyo anawataka wasanii wabadili mfumo wao wa maisha kwa kuachana na mambo maovu, anasa za dunia kwani hawajui siku wala saa ya kufariki dunia.
“Wasanii tunazidi kufa, juzi tumemzika Ngwea, leo tena Kashi wasanii tunatakiwa kufanya ibada, wenye sauti za kuimba wamwimbie Mungu kwani waliotangulia hawakujua kama watakufa, binafsi nimeanza kusali tangu nilipofiwa na mama yangu,alisema Dude.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post