Naibu waziri wa Nchi Twala za Mikoa na serikali za Mitaa ambae Pia ni ,Mbunge wa ji mbo la Ruangwa akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Nassor Ally Hamid wakati wa mapumziko
mafupi ya Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Lindi.Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila akifunga kikao cha bodi ya Barabara MkoaWenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Lindi wasikiliza kwa makini kikao cha Bodi ya BarabaraWakuu wa wilaya za mkoa wa Lindi
Na Abdulaziz Video,Lindi
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali
za mitaa [TAMISEMI] Kassim Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa amewataka wanasiasa mkoani Lindi kuacha tabia ya kuwa chanzo cha kuchochea vurugu katika jamii badala yake washirikiane na watendaji na wananchi ili kuinua mkoa huo ambao uko nyuma kimaendeleo.
Naibu waziri huyo ametoa wito huo wakati alipokuwa anazungumza na wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri mkoa [RCC] katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Lindi.
Alisema kazi kubwa ya wanasiasa ni kutembelea wananchi kwa lengo la kuwasikiliza kero zao ,kuwahimiza na kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao ili kuchochea maendeleo na sio kuchochea kufanya vurugu na kusababisha kuvunjika kwa amani.
Wanasiasa wamekuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao kwa kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo badala ya kushiriki vurugu.
“sio vyema wanasiasa waliochaguliwa na wananchi kwa ajili ya kusimamia na kuwawakilisha wakatumia nafasi hiyo majukwaani kutamka maneno ya uchochezi na kusababisha kupotea mwelekeo wa kuwaletea wananchi wake maendeleo hii inaonesha usivyotosha kwa wapiga kura; alimalizia Majaliwa
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.