Staa wa ngoma still a liar, Wahu Kagwi kutoka Kenya ni mjamzito, na anategemea kupata mtoto wake wa pili mwezi August mwaka huu.
Wahu ambaye pia ni mke wa David Mathenge, a.k.a Nameless anatuhabarisha kwamba anategemea kuachia ngoma yake nyingine mwishoni mwa wiki hii, ngoma ambayo mwenyewe anaitabiri kwamba itatikisa Afrika Mashariki yote.
Mashabiki wa mwanamuziki huyo ambaye wakati anapata mtoto wake wa kwanza aliachia ngoma ya Sweet Love, wanaitabiri ngoma hiyo kushika kweli kutokana na hisia kwamba Wahu anapokuwa katika ujauzito huwa anakuwa na hisia kali za kuandika kuliko akiwa katika hali ya kawaida.
Jumanne hii Wahu aliulizwa na shabiki wake iwapo ana ujauzito, na alijibu kwa mkato tu, "Yes I am".
Tags
HABARI ZA WASANII