Unknown Unknown Author
Title: 'Wakati wa kula Wadudu ni sasa' UN
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ulaji zaidi wa wadudu huenda ukasaidia dunia kukabiliana na uhaba wa chakula, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na umoja wa Mataifa. ...

Ulaji zaidi wa wadudu huenda ukasaidia dunia kukabiliana na uhaba wa chakula, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na umoja wa Mataifa.

Ripoti hiyo iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo na UN, inasema kuwa kula wadudu huenda kukasaidia kuboresha afya na kupunguza idadi ya watu.

Kadhalika ripoti hiyo inasema kuwa zaidi ya watu bilioni mbili duniani hula wadudu kama sehemu ya lishe bora.

Hata hivyo inasema kukerwa kwa watu na kuwaona wadudu ndicho kinasalia kuwa kikwazo kikubwa katika nchi nyingi za Magharibi.

Nyingu au (Wasp), Beetle pamoja na wadudu wengine, hawatumiki sana kama chakula kwa binadamu au wanyama, kulingana na ripoti hiyo.

Kilimo cha kufuga Wadudu ni moja ya njia za kusuluhisha tatizo la uhaba wa chakula

"wadudu wako kila mahali, na kuzaana kwa haraka, na pia hukuwa kwa haraka sana pamoja na kuwa na athari ndogo sana kwa mazingira,'' ilisema ripoti hiyo.

Thamani ya wadudu kwa afya.

Waandishi wa ripoti hiyo wamesema kuwa, wadudu wanaleta afya nzuri , wakiwa na viwango vya juu vya Proteni , mafuta na madini mengine.

''Wana umuhimu mkubwa kwa kuwa na uwezo wa kuongeza madini mwilini, hasa kwa watoto wenye utapia mlo.''

Wadudu pia ni muhimu sana kwa sababu wanakula chakula kidogo kuliko wanyama. Mfano Chenene (cricket) wanakula chakula kidogo sana ikilinganishwa na mifugo ingawa wana viwango sawa vya madini ya Proteni.

Aidha wadudu hao pia wana athari ndogo sana katika uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa na mifugo.

Gesi aina ya Ammonia inayotolewa na wadudu kadhaa, ni ya chini mno ikilinganishwa na ile inayotolewa na mifugo mfano Nguruwe.

Ripoti hiyo inataka mikahawa kuwa na wadudu miongoni mwa vyakula wanavyouza.

Wadudu huliwa na watu wengi duniani lakini dhana hiyo haiwezi kufanikishwa kwa watu wa nchi za Magharibi.

Ripoti hiyo inapendekeza kuwa sekta ya chakula inaweza kusaidia katika kuhamasisha watu kubadili wanavyokula na hata kuonyesha watu kuwa wanaweza kula baadhi ya vyakula.

Katika sehemu kadhaa duniani wadudu kadhaa huonekana kama chakula kitamu.

Mfano Viwavi huliwa Kusini mwa Afrika na huonekana kama chakula cha hadhi ya juu na pia huuzwa kwa bei ghali.

Wadudu wengi wanaoliwa hutolewa msituni na hutumiwa na watu maalum.

Ripoti hiyo Inapendekeza kuwepo sheria ya kudhibiti uzalishaji wa wadudu kama chakula.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top