ROBBEN AIBEBESHA UBINGWA WA ULAYA BAYERN KWA BAO LA DAKIKA YA 89 WEMBLEY

clip_image001Bao la ubingwa: Arjen Robben amekuwa shujaa wa fainali ya Ligi ya Mabingwa usiku huuclip_image002[6]Mfungaji wa bao la kwanzaTop of the pile: Bayern Munich are the Champions of Europe for a fifth time after beating Borussia DortmundBayern Munich wakisherehekea taji lao la Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga Borussia Dortmund

WINGA Arjen Robben ameuzika mzimu wa kukosa penalti msimu uliopita katika fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea, baada ya usiku huu kuifungia bao la ushindi Bayern Munich katika fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Wembley, London, England ikishinda 2-1 na kutwaa Kombe hilo.

Bayern sasa wanakuwa mabingwa wapya wa Ulaya, wakirithi taji lililoachwa wazi na Chelsea kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Wajerumani wenzao, Borussia Dortmund katika mchezo mkali na wa kusisimua.

Mholanzi huyo alifunga bao hilo tamu dakika ya 89, baada ya awali kipindi cha kwanza kukosa mabao mawili ya wazi. Lakini ndiye aliyetoa pasi ya bao la kwanza kwa Bayern lililofungwa na Mario Mandzukic dakika ya 60.

Dortmund ilisawazisha kwa penalti baada ya Dante kumuangusha kwenye eneo la hatari Marco Reus na Ilkay Gundogan akaenda kufunga dakika ya 67.

Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Nicola Rizzoli  kutoka Italia, kikosi cha Bayern kilikuwa; Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Javi Martinez, Schweinsteiger, Robben, Muller, Ribery/Gustavo dk90+1 na Mandzukic/Gomez dk90+4.

Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender/Sahin dk90+1, Gundogan, Blaszczykowski/Schieber dk90+1, Reus, Grosskreutz na Lewandowski.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post