RAIS REAL ATANGAZA RASMI KUONDOKA KWA MOURINHO!

clip_image002Rais wa Real Madrid Florentino Perez leo ametangaza kuondoka kwa Kocha wao Mkuu Jose Mourinho kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.

Akihutubia Wanahabari waliojazana, Perez alisema: “Tumeamua kumaliza uhusiano wetu. Hakuna Mtu aliefukuzwa kazi, ni makubaliano ya pande mbili.”

Wakiwa wamebakisha Mechi 2 za La Liga, Real Madrid wako Nafasi ya Pili na Pointi 13 nyuma ya Mabingwa FC Barcelona na Ijumaa iliyopita walitwangwa 2-1 kwenye Fainali ya Copa del Rey na Mahasimu wao Atletico Madrid.

clip_image001Katika Miaka mitatu aliyodumu Real, Mourinho alishindwa kuivusha Real zaidi ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kutolewa katika hatua hiyo katika Misimu yote hiyo na Msimu huu ilishikishwa adabu na Borussia Dortmund kwa kuchapwa Bao 4-1 huko Germany na wao kujitutumua na kushinda 2-0 Nyumbani kwao.

Kabla Mourinho kutua Real Madrid, Klabu hiyo ilikaa Miaka miwili bila Taji lolote na alipofika yeye wakatwaa Copa del Rey Mwaka 2011 na kufuatia Ubingwa wa Spain wa La Liga Mwaka 2012 lakini Msimu huu ametoka patupu ukiachia Super Cup.

Inaaminika Jose Mourinho anarudi Klabu yake ya zamani huko England, Chelsea, na hapo Real atatua Carlo Ancelotti kutoka PSG ingawa haujapatikana uthibitisho rasmi mbali ya PSG kumkatalia Ancelotti kuhama.

MOURINHO NA MATAJI:

UCL: 2004 (Porto), 2010 (Inter Milan)

UEFA CUP: 2003 (Porto)

PRIMEIRA LIGA: 2003, 2004 (Porto)

TACA DE PORTUGAL: 2003 (Porto)

BPL: 2005, 2006 (Chelsea)

FA CUP: 2007 (Chelsea)

LEAGUE CUP: 2005, 2007 (Chelsea)

SERIE A: 2009, 2010 (Inter Milan)

COPPA ITALIA: 2010 (Inter Milan)

COPA DEL REY: 2011 (Real Madrid)

LA LIGA: 2012 (Real Madrid)

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post