Unknown Unknown Author
Title: TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YAKATALIWA LUPEMBE NJOMBE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Diwani wa Kata ya Lupembe Bi Twilumba Wapalila katikati Amesema Baada ya Kuahirishwa Kwa Mkutano Huo Sasa Mkutano Mwingine Utafanyika Jumamo...

clip_image001Diwani wa Kata ya Lupembe Bi Twilumba Wapalila katikati Amesema Baada ya Kuahirishwa Kwa Mkutano Huo Sasa Mkutano Mwingine Utafanyika Jumamosi Wiki Ijayo.clip_image001[4]Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Wilaya ya Njombe Bwana Lupyana Fute[Jacky's]Aliyevalia Shati la CCM Ambaye Pia ni Diwani wa Kata ya Njombe Mjini awali aliuagiza uongozi wa Kijiji kuwasomea Wananchi Taarifa ya Mapato na Matumizi Kila baada ya Miezi Mitatu Jambo ambalo halitekelezeki.

Na Michael Ngilangwa.

Wananchi wa Kijiji Cha Lupembe Barazani Wilayani Njombe Wameikataa Taarifa ya Mapato na Matumizi Iliosomwa na Uongozi wa Kijiji Hicho Wakati wa Mkutano Uliofanyika  Kijijini Humo,Kwa Madai ya Taarifa Hiyo Kuwa na Mapungufu Mengi.
Miongoni Mwa Mapungufu Hayo ni Pamoja na Taarifa Hiyo Kutoainisha Kikamilifu Kuhusu Matumizi ya Fedha Za Kijiji Pamoja na Wananchi Kutokubaliana na Mchanganuo wa Fedha Hizo Kama Ulivyoainishwa na Viongozi Wakati wa Mkutano Huo.

Aidha Kutokana na Hali Hiyo,Uongozi wa Kijiji Ulilazimika Kurudisha Kiasi Cha Shilingi Millioni Mbili Ambazo Hazikuweza Kupatiwa Majibu ya Kina Licha ya Wananchi Kuhoji Mara Kadhaa Kuhusu Fedha Hizo Ambazo Zilitengwa Kwaajili ya Kuboresha Miundombinu ya Maji.
Akizungumza na blog hii , Diwani wa Kata ya Lupembe Bi Twilumba Wapalila Amesema Baada ya Kuahirishwa Kwa Mkutano Huo Sasa Mkutano Mwingine Utafanyika Jumamosi Wiki Ijayo na Kuongeza Kuwa Wanatarajia Kuzisoma Taarifa Zote Kama Ilivyoelekezwa na Wananchi na Viongozi Mbalimbali wa Chama na Serikali.
Akiwa Kwenye MKutano wa Hadhara Wakati wa Ziara ya Kutembelea Vijiji Vya Tarafa ya Lupembe, Mjumbe wa NEC Taifa Wiilayani Njombe Bw Lupyana Fute Aliuagiuza Uongozi wa Kijiji Hicho Kuhakikisha Unawasomea Wananchi Taarifa za Mapato na Mtaumizi Hadi Kufikia May 18 Mwaka Huu na Kusema Kinyume na Hapo Hatua za Kisheria Zingeweza Kuchukuliwa Kwa Viongozi Hao.
Kumekuwa na Hali ya Viongozi wsa Vijiji Mkoani Njombe Kukiuka Sheria za Serikali za Mitaa Zinazowataka Kuwasomea Wananchi Taarifa za Mapato na Matumizi Kila Baada ya Miezi Mitatu Jambo Ambalo Limekuwa Likisababisha Migogoro ya Mara Kwa Mara Baina ya Wananchi na Viongozi Wao.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top