Unknown Unknown Author
Title: MTANZANIA ATWAA MEDALI YA DHAHABU, ROMANIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Imani Makongoro, Mwanariadha wa Tanzania, Mary Naali ametwaa medali ya dhahabu mbio za nusu marathon (km 21) ‘Bucharest International H...

clip_image002

Na Imani Makongoro,

Mwanariadha wa Tanzania, Mary Naali ametwaa medali ya dhahabu mbio za nusu marathon (km 21) ‘Bucharest International Half Marathon’ zilizofanyika nchini Romania.

Naali anayetokea klabu ya African Ambassadors Athletics (AAAC) ya Arusha alitumia saa 1:16:32 kumaliza mbio hizo zilizokuwa na ushindani mkubwa.

Mkimbiaji wa Ethiopia, Salome Albere alikamata nafasi ya pili akitumia saa 1:18:20, wakati Nicoleta Petrescu wa Romania akishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 1:20:24 kumaliza mbio hizo.

Mkenya Kirui Nicholas aliibuka kinara upande wa wanaume kwenye mbio hizo akitumia saa 1:04:07 na Andrew Lesuuda aliyetumia saa 1:04:53 na Japhet Kanda aliyetumia saa 1:07:12 wote kutoka Kenya wakihitimisha tatu bora.

“Medali hii ni zawadi kwa taifa langu, nimepambana hadi mwisho kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri japo ushindani ulikuwa mkali,” alisema Naali.

Naali anashikilia rekodi ya kutwaa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika New Delhi, India mwaka 2010.
Source; mwananchi

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top