Wladimir Klitschko akiwa amepozi na mikanda yake baada ya kumdunda Francesco Pianeta
BONDIA Wladimir Klitschko amempa somo David Haye usiku huu baada ya kumpiga bondia ambaye alikuwa hajawahi kupigwa, Francesco Pianeta kwa Knockout (KO) katika raundi ya sita kwenye pambano la uzito wa juu mjini Mannheim.Ulikuwa ushindi wa 51 wa KO kwa Klitschko akiwa bingwa wa WBA, WBO, IBF na IBO akiendeleza rekodi yake ya kupigana mapambano 60 na kupoteza matatu tu.
Haye atapigana na Charr mjini Manchester Juni 29 akiwa na dhamira ya kupigana na Wladimir au Vitali Klitschko akishinda pambano hilo kuwania taji la WBC.
Haye alipigwa kwa pointi na Wladimir mjini Hamburg Julai mwaka 2011.
Kimada wa Klitschko, mwigizaji Hayden Panettiere akifuatilia pambano
Klitschko na Pianeta

Refa akimuhesabia Pianeta baada ya kudondoka raundi ya sita

Tags
SPORTS NEWS