Afisa Utamaduni wa Manispaa ya lindi ndie alikuwa mgeni rasmi wa Mchezo wa leo (Kariakoo Fc 3 – Kusini Soccer 0).
Bechi la ufundi la timu ya Kariakoo Fc, mechi na Kusini soccer (Kariakoo Fc 3 – Kusini Soccer 0).
Bechi la ufundi la timu ya Kusini Soccer, mechi na Kariakoo Fc(Kariakoo Fc 3 – Kusini Soccer 0).
Waamuzi wa Mechi ya leo kati ya Kariakoo Fc na Kusini Soccer zote za mjini Lindi.
NA: Fungwa K, Lindi
Timu ya Kariakoo FC ikianza vyema mashindano ya Ligi ya Mkoa Hapa mjini lindi iliikaribisha Timu ya Kusini Soccer katika uwanja wa ILULU Timu hizi zikiwa na upinzani mkubwa Mjini hapa.
Mchezo huo ulioanza kwa matatizo ya Jezi kufanana na Waamuzi ambapo Timu ya Kariakoo Fc ilifanana Jezi na Waamuzi wa Leo na Kuamriwa Ibadilishe jezi na wao kuanza kugoma, Mjadalahuo ulijukua Takribani Dakika 30 na Ndipo Timu ya Kariakoo Fc ikabidi iadhime Jezi kutoka Kwa timu ya Lindi Sports ya Mjini hapa.
Mchezo ulianza kwa Kasi huku Kariakoo Fc wakionesha kuwa wao wamedhamiria kuchukua point tatu za mechi hii kwa kuanza kulishambulia lango la Kusini Soccer Mara kadhaa.
Ni Salum Abdillah aliewainua Mashabiki wa Kariakoo Fc kwa Goli zuri ambalo lilitokana na Mabeki wa Kusini Kujichanganya na kumuachia mpira Salum na kuuweka Kimiani. Hata hivyo Kusini walijitahidi kutafuta bao lakini ngome ya ulinzi ya Kariakoo Fc ilikuwa barabara ambayo iliongozwa na kampteni wao Anafi. Burudani ya kandanda safi iliendelea na bila kumsahau Mshambuliaji machachari Nasoro Cholo hakufanya ajizi pale alipopewa pasi nzuri na kuiandikia timu yake ya Kariakoo goli la pili katika kipindi hicho cha Kwanza.
Kipindi chapili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya hapa na pale ilikukabiliana na mwenendo wa mchezo, Kariakoo Fc iliweza kupata tena Goli la Tatu kupitia mshambuliaji wake Nasoro Cholo ikiwa ni goli lake la pili katika Mashindano haya. hadi mwisho wa mchezo Kariakoo Fc 3 Kusini Soccoer 0.
Tags
SPORTS NEWS