Nyota huyo wa Wales, ambaye ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kandanda England, amekuwa katika msimu mzuri, akitoa mchango mkubwa kwa Spurs.
Akiwa amefunga mabao 19 katika mechi 29 za Ligi Kuu England, Bale ameendelea kuzikuna klabu kubwa, zikiwemo Real Madrid na Bayern Munich ambazo zinaitaka saini yake kwa gharama yoyote.
Pamoja na hayo, Villas-Boas amejibu leo, akisema: "Hata kama kiwango hicho cha fedha kinamlenga mchezaji huyo, haijalishi kwetu, kwa sababu ni mchezaji wetu na mchezaji ambaye tunatakiwa kuendelea kuwa naye kuhakikisha tunatimiza malengo yetu na kuendeleza harakati.
"Taarifa nilizonazo kutoka kwenye klabu klabu ni kwamba, mchezaji huyo yupo hapa kubaki, hata ikiwa tutapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa au la. Klabu lazima iendelee mbele kwa kuwashikilia wachezaji wazuri,".
Tags
SPORTS NEWS