Unknown Unknown Author
Title: BINGWA EUROPA LEAGUE KUFUZU MOJA KWA MOJA LIGI YA MABINGWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
BINGWA wa Europa League atafuzu moja kwa moja kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia msimu wa 2015-16. Mpango huo wa UEFA umelenga kuyapati...

clip_image002BINGWA wa Europa League atafuzu moja kwa moja kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia msimu wa 2015-16.

Mpango huo wa UEFA umelenga kuyapatia umaarufu mashindano yake hayo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu, ambayo Chelsea ilitwaa taji lake mapema mwezi huu.

Inafahamika kwamba, bingwa wa Europa League na Ligi ya Mabingwa hawawezi kucheza michuano hiyo iwapo watakosa nafasi kupitia ligi za nchini mwao.

Chelsea ilitwaa taji baada ya kuifunga Benfica kwa bao la dakika za lala salama la Branislav Ivanovic lililotengeneza ushindi wa 2-1 dhidi ya klabu hiyo ya Ureno.

Chelsea wakishangilia taji lao la Europa League baada ya kuifunga 2-1 Benfica.

MABINGWA WA EUROPA LEAGUE
(Waliowekewa * hawakufuzu Ligi ya Mabingwa) 

MWAKA BINGWA
2013 Chelsea
2012 Atletico Madrid*
2011 Porto
2010 Atletico Madrid*
2009 Shakhtar Donetsk*
2008 Zenit St Petersburg
2007 Sevilla
2006 Sevilla*
2005 CSKA Moscow*
2004 Valencia
Zote Chelsea na Benfica zilitolewa katika Ligi ya Mabingwa  na kushindwa kuvuka hatua ya makundi.
Sheria mpya itamaanisha England inaweza kuwa na timu tano katika Ligi ya Mabingwa msimu wa 2015-16 kama moja ya klabu zake itabeba taji la Europa League mwaka 2015 na kumaliza nje ya Nne Bora katika Ligi Kuu.
Wigan, Swansea na Tottenham wataiwakilisha England katika Europa League msimu ujao.
Wakati huo huo, UEFA imepitisha adhabu ya mechi 10 kwa mechi za Ulaya, iwapo mchezaji au kiongozi anakutwa na hatua ya ubaguzi. 
Ubaguzi wa mshabiki utaiponza timu kucheza na mashabiki wachache kwa hatua ya kwanza ya usalama na kufungwa kwa Uwanja mzima kwa hatua ya pili ya usalama.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top