BAYERN YAITANDIKA BARCA 3–0 CAMP NOU NA KUFUZU KWA JUMLA YA 7-0

Fussball's coming home: Bayern secured an all-German Champions league final against Borussia Dortmund
Itakuwa fainali ya Wajerumani watupu Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Wembley wiki tatu zijazo Jumamosi, ikiwakutanisha Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Hiyo inafuatia Barcelona iliyomkosa Lionel Messi aliyekuwa benchi kutandikwa mabao 3-0 nyumbani usiku huu, baada ya awali kuchapwa 4-0 Ujerumani, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 7-0.
Barcelona walionekana kabisa kuzidiwa uwezo na mapema tu walionekana hawawezi kupanda mlima huo. Mabao ya Bayern ambao tayari ni mabingwa wa Ujerumani, wakiivua taji Dortmund, yamefungwa na Arjen Robben dakika ya 49, Gerard Pique aliyejifunga dakika ya 72 na Thomas Muller dakika ya 76.

Kikosi cha Barca leo kilikuwa; Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra/Montoya dk87, Adriano, Xavi/Sanchez dk55, Song, Iniesta/Thiago dk64, Villa, Fabregas na Pedro.
Bayern Munich: Neuer, Lahm/Rafinha dk77, Boateng, Van Buyten, Alaba, Javi Martinez/Tymoschuk dk74, Schweinsteiger/Gustavo dk66, Robben, Muller, Ribery na Mandzukic.
No stopping that: Robben (unseen) cut inside and curled a brilliant finish into the far corner of Barca's netRobben (haonekani) shuti lake likitinga nyavuniHamstrung: Lionel Messi (right) was left on the bench despite Barca's need to overturn a four-goal deficitLionel Messi (kulia) alibaki benchi licha ya Barca kutakiwa kupiku kipigo cha mabao manne mchezaji huyu anasumbuliwa na Nyama za pajaHang your head: Barca goalkeeper Victor Valdes screams in frustration after Pique's gaffeKipa wa Barca, Victor Valdes akilalamika baada ya Pique kujifungaSalt in the wounds: Bayern's Thomas Muller (centre left) headed in a third goal late onThomas Muller wa Bayern akifunga bao la tatuLondon calling: Bayern Munich goalkeeper Manuel Neuer (left) and his team-mates have a final dateKipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer (kushoto) na wachezaji wenzake wametinga fainaliWhat's gone wrong? Gerard Pique, David Villa and Cesc Fabregas were left scratching their headsGerard Pique, David Villa na Cesc Fabregas wakitafakari kipigo





Previous Post Next Post