Wadau mbalimbali wa Serikali,Wafanyabiashara na wanahabari toka Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma wanakutana leo katika warsha ya mashirikiano ya kibiashara kwa mikoa hiyo wanakutana leo ili kujenga na kubadilishana mawazo kwa lengo la kujenga uelewano na Ushirikiano ambao utasaidia kutekeleza Dira ya kibiashara kwa Ufanisi
Majadiliano hayo ya ushirikiano yatachangia katika kusukuma mbele utekelezaji wa Dira ya Tanzania ya Maendeleo 2025 pamoja na juhudi mbalimbali kuendelea utekelezaji wa Dira hiyo hauendani na shabaha ya kuiwezesha nchi ya kipato cha kati inayojivunia maendeleo makubwa na maisha bora ya wananchi.
Katika warsha hii mada kuu ni kuhamasisha Teknolojia kwa mageuzi ya kiuchumi na kijamii Tanzania itawasilishwa ikienda sambamba na mada ndogondogo ikiwemo Umuhimu wa Ubunifu katika mageuzi ya kiuchumi na kijamii, Mchango wa Tehama, Ubora wa Viwango katika wilaya, usalama wa watu na mali zao ikiwa pamoja na majadiliano ya Vikundi mada ambazo zitatolewa na UDSM,COSTECH,TCRA,TBS na Polisi Makao Makuu.
Tags
HABARI ZA KITAIFA