Badhi ya Abiria wakiwa kituo cha mabasi mjini Lindi bila kuelewa hatma ya safari yao hii leobaadhi ya mabasi yaendayo mtwara yakiwa mjini Lindi toka jana baada ya mgomo huo kuhofia usalamaKAMANDA wa Polisi mkoa wa Lindi George Mwakajinga akiwasihi madereva kuridhia kusindikizwa na polisi kwenda mtwara
Zaidi ya Abiria 400 Waliokuwa wanafanya safari kati ya Dar es sallam
jana walilazimika kusitishiwa safari mkoani Lindi kufuatia madereva na
wamiliki wa Mabasi waliyokuwa wanasafiria kuogopa kutokana na hali ya Amani kutokuwepo Mkoani Mtwara kufuatia Vurugu za Mgogoro wa Gesi zilizokuwa zikiendelea Juzi na Jana mkoani huko
Lindi Yetu Ilifika katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Lindi na
kukuta msongamano Huo ambapo Jeshi la Polisi Mkoani Lindi likiongozwa na kamanda wa Polisi wa Mkoa George Mwakajinga liliamuamua kutoa ulinzi kwa mabasi hayo kuyafikisha Mtwara hali ambayo ilikataliwa na Madereva wa Mabasi pamoja na baadhi ya Abiria.
Kamanda Mwakajinga akiongea na blog hii alieleza kuwa sambamba na kuwahakikishia Usalama wa mabasi hayo kwenda Mtwara alishangazwa na baadhi ya madereva kugoma kusindikizwa na Polisi kwa hofu ya Usalama wa Magari na Abiria wanaowasafirisha
Mwandishi hakika Jeshi limejipanga kuwasindikiza hadi mtwara ila
nimepigwa na butwaa baada ya abiria na Madereva kugoma kwenda mpaka sasa sijui tufanye nini maana sasa ni mgomo huu ila nakuhakikishia bado tutawapa Ulinzi wa Kutosha na watakuwa salama
Baadhi ya Madereva wa Mabasi hayo walieleza hofu yao kuhusu kuendelea na safari huku baadhi ya Abiria wakiwa na misimamo Tofauti kuhusiana na Hali hiyo Ambapo wengine walilazimisha kusafiri huku wengine wakihofia usalama wao huku madereva wakikataa kuondoka Lindi Mmiliki wa mabasi ya Buti la Zungu, Zubeiry Namachokole jana aliamua kutoa gari yake nyingine aina ya Coaster kuwapeleka abiria wake waliolala Lindi, badala ya Basi yake ya Yutong kuhofia usalama wa Basi hilo.
Hadi tunakwenda Mitamboni abiria wengi walikuwa wakihangaika kwa makondakta na Madereva huku wakitafuta msaada wa Serikali ili
wasaidiwe chakula na hifadhi hadi hali itakaporejea kuanza safari
kutokana na wengi kusafiri wakiwa na hali ngumu wakiwemo akina mama na watoto
Baadhi ya Mabasi hayo leo yameanza safari mjini Lindi kurejea Dar es salaam
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.