Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Afisa mkuu wa mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota amesema, baada ya kujitambulisha sokoni kwa Intanet isiyo na kikomo ya BANJUKA leo tunazonfua huduma mpya ujulikanayo kama BANDO NA TTCL. Huduma hii itamuwezesha mteja kufaidika na meseji za bila kikomo, kuperuzi intanet na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa wakati mmoja kwa bei hadi ya shilingi 500.
Amesema BANDO NA TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phone za TTCL zinazopatikana katika vituo vyetu vya huduma kwa wateja nchini.
Bw. Ngota amesema TTCL pia imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile intanet kwa kampeni ya BASTI ikimaanisha peruzi intanet zaidi kwa gharama nafuu. Ametolea mfano kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000/= sasa kinauzwa kwa shilingi 25,000/= tu. Hii ni nafasi si tu kwa wateja waliopo wa TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu, bali hata wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga na mtandao wa TTCL. (haki ya mawasiliano kwa wote).
Amesisitiza kuwa , BANDO NA TTCL na kampeni ya BASTI zina manufaa mengi ikiwa ni pamoja na huduma ya mobile intanet kwa gharama nafuu, vifurushi vya siku, wiki na mwezi kulingana na mahitaji yako, mobile intanet yenye ubora na kasi ya juu zaidi.
Amesema kwa kununua modem ya TTCL kwa sh 29,000/= utapata 2GB bure kuperuzi intanet na kukupa thamani bora kwa pesa yako.
‘Leo hii wateja wengi zaidi na hasa wanafunzi na wajasiriamali wanatumia simu za kisasa (smart phones, tablet PC’s kama iPad, Samsung Galaxy nk) na kompyuta ili kupata huduma za intaneti na mitandao ya kijamii kwa shughuli zao za kila siku.’
Aidha, kuwepo kwa mitandao ya mawasiliano ya baharini ya EASSy na SEACOM katika Pwani ya Tanzania, mkongo wa Taifa wa mawasiliano na mtandao wake ulionenea nchi nzima umeiwezesha TTCL kuwa mstari wa mbele kutoa huduma za mawasiliano ikiwamo intaneti kwa ofisi za serikali na benki mbalimbali hapa nchini.
Mkongo wa Taifa umesaidia kuwa na huduma bora zaidi ambapo kwa sasa wananchi wanaweza kupata huduma nyingi zikiwemo matibabu mtandao, elimu mtandao, biashara mtandao na Serikali mtandao, Benki – Mtandao, Pesa – mtandao na pia kufanikiwa kuifikisha Tanzania katika nchi za Zambia, Burundi, Rwanda na Malawi kwa huduma za mawasiliano.
Tags
HABARI ZA KITAIFA