Dc Kilwa aagiza watendaji kutoa huduma kwa jamii kwa Muda Muafaka

ULEGA -DC KILWAAbdallah Ulega ambaye ni Mkuu wa Wilaya Kilwa Mkoa wa Lindi akiongea na Watendaji wakati wa ziara yake  ya Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo Wilayani Kilwa.
ADDO MAPUNDAAddo mapunda, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa
Na Abdulaziz,LindiMKUU wa wilaya Kilwa Mkoani Lindi Abdala Ulega ameeleza kuwa wakati umefika sasa kwa watendaji na viongozi wa umma kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi bila ya kuwapangia muda maalumu wa kuonana nao.Hayo yalibainika katika ziara mbalimbali za kukagua miradi ya
maendeleo katika kata mbalimbali za Wilaya hiyo .
Ulega akiongea na baadhi ya watendaji amewaasa kuacha urasimu wa
utoaji wa huduma kwa jamii na kubainisha kuwa Watendaji na watoa
huduma mbalimbali za jamii kuwa vikwazo hali inayochangia wananchi kukosa imani na serikali yao kutokana na vitendo/taratibu za kuwahudumia wananchi ikiwemo kuwapangia muda maalumu wa kuonana nao kupata huduma stahiki hali ambayo ni moja ya vikwazo

vinavyolalamikiwa sana Wilayani Humo .
‘Mtumishi wa umma ni Yule aliyetayari kuwahudumia wananchi kwa
misingi ya haki, unyenyekevu nidhamu na uadilifu asiyekuwa tayari
kufanya hivyo aamue kuacha kazi na kabla ya watu kuichukia na
kuisema vibaya serikali yao wale wote watakao fanya kazi kwa mazoea na kutotenda haki kwa katika kutoa huduma kwa wakati wawajibike kabla hawajawajibishwa kwa sababu Hatuwezi kukubali kuona serikali ikitukanwa na kupakwa matope kwa uzembe na makosa ya mtendaji mmoja ambaye hataki kuwajibika” alisema Ulega.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Addo Mapunda akiongea na Globu hii alibainisha kuwa ofisi yake imejipanga kuhakikisha Jamii  zinapata huduma stahiki zinazotolewa na Halmashauri hiyo na kuahidi kueleza kuwa kipo kitengo cha kupokea Kero na Malalamiko ili kutafutiwa ufumbuzi
‘Mwandishi nakuhakikishia Maagizo ya Mkuu wa Wilaya kuhusu watendaji ninayashughulikia ipasavyo na ndio maana naalika watendaji wa kata wote na maafisa Tarafa wote kila kukiwa na Baraza la Madiwani ili nao wafikishe ujumbe kwa wananchi wao maazimio yote yanayotolewa na kupitishwa na Madiwani’Aidha Mapunda alisisitiza kuwa Ofisi yake imejipanga kuhakikisha Elimu inayotolewa wilayani humo Inaboreka ili kuondoka na aibu ya Wilaya hiyo kuwa ya mwisho na kutoa wito kwa jamii kushirikiana vema na Walimu waliopangwa katika shule zao ikiwa pamoja na kuanza kujenga nyumba bora kusaidia watumishi wanaoletwa kwa Kushirikiana ili walimu hao wafurahie kuishi.
Previous Post Next Post