MANCHESTER UNITED YAWEZA KUTANGAZA UBINGWA WA BPL JUMATATU

MABINGWA watetezi wa BPL, Barclays Premier League, Manchester City huenda Jumatatu Usiku wakapokonywa Taji lao ikiwa Jumapili watafungwa na Tottenham Uwanjani White Hart Lane na Manchester United kuifunga Aston Villa Jumatatu Usiku Uwanjani Old Trafford.

RATIBA IKO HIVI:

JUMAMOSI SAA 11: 00 JIONI :

FULHAM v ARSENAL, Norwich v Reading, QPR v Stoke,  Sunderland v Everton, Swansea v Southampton, West Brom v Newcastle,

West Ham v Wigan

JUMAPILI SAA 9:30 Mchana:

SPURS v MAN CITY!

SAA 12: 00 JIONI

LIVERPOOL v CHELSEA,

JUMATATU SAA 4:00 USIKU:

MAN UNITED v ASTON VILLA!

Raha ya Mechi za Wikiendi hii katika kuwania 4 Bora ni kuwa Jumamosi Arsenal wataanza kucheza ugenini huko Craven Cottage dhidi ya Fulham na ushindi kwao utaleta mchecheto kwa Chelsea ambao Jumapili wapo Anfield kucheza na Liverpool na White Hart Lane ni mtanange kati ya Tottenham na Man City.
Jumamosi, Sunderland, chini ya Meneja mpya Paolo Di Canio, mara tu baada ya kutoka kuichapa Newcastle ugenini, watakuwa Nyumbani Stadium of Light kuivaa Evverton.
Mechi nyingine ya nvutano ni kati ya Marafiki, Sam Allardyce na Tony Pulis, wakati West Ham watakapocheza na Wigan.

MSIMAMO-TIMU ZA JUU
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Man United 33 26 3 4 75 35 40 81
2
Man City
32 20 8 4 58 27 31 68
3 Chelsea 32 18 7 7 64 33 31 61
4 Arsenal 33 17 9 7 64 35 29 60
5 Tottenham 32 17 7 8 55 40 15 58
6 Everton 33 14 14 5 51 37 14 56
7 Liverpool 33 13 11 9 59 40 19 50
Man City wako Ponti 13 nyuma ya Man United ambao wako kileleni lakini Mechi yao City na Tottenham ni ngumu mno kwani Tottenham wanapigana na Chelsea, Arsenal na Everton kuwania 4 Bora ili kucheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
MECHI ZA LIGI ZILIZOBAKI:
MAN CITY
[PTS 68, MECHI BADO 6]
MAN UNITED
[PTS 81, MECHI BADO 5]
Tottenham v Man City
Man City v West Ham
Swansea v Man City
Reading v Man City
Man City v Norwich
Man City V West Brom
21 Apr
27 Apr
4 Mei
12 Mei
19 Mei
?????
Man Utd v Aston Villa
Arsenal v Man Utd
Man Utd v Chelsea
Man Utd v Swansea
West Brom v Man Utd
22 Apr
28 Apr
5 Mei
12 Mei
19 Mei


Previous Post Next Post