Van Persie alipiga Hat-trick hiyo ndani ya dakika 33 za mechi hiyo, likiwemo bao lililoingia kwenye kinyang'anyiro cha bao bora la msimu alipounganisha moja kwa moja pasi ndefu ya Wayne Rooney akiwa nje kidogo ya eneo la hatari.
Mdachi huyo, aliyeamua kujiunga na kikosi cha Sir Alex Ferguson badala ya Manchester City ya Roberto Mancini msimu huu akitokea Arsenal, alifunga mabao yake katika dakika za pili, 12 na 33, mawili pasi za Rooney na moja pasi ya Ryan Giggs.
Ferguson leo alichezesha viungo watatu katikati, Shinji Kagawa, Michael Carrick na Rooney aliyekuwa akiichezesha timu mbili na kufanya kazi nzuri ya kupendeza, akitoa pasi mbili za mabao kabla ya kumpisha Danny Wellbeck dakika ya 72.
Kikosi cha Man United leo kilikuwa; De Gea, Rafael, Evra, Jones, Evans, Valencia, Giggs, Carrick, Kagawa, Rooney/Welbeck dk72 na Van Persie
Aston Villa; Guzan, Vlaar, Bennett/Clark dk80,Baker, Lowton, N'Zogbia/El Ahmadi dk46,Westwood, Delph, Agbonlahor, Benteke na Weimann
Tags
SPORTS NEWS