Kitaifa. Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika katika kata ya Mingoyo shule ya msingi Mnazi mmoja Lindi
Maadhimisho hayo yalizindiliwa jana kitaifa mkoani Pwani na Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete yatatumika katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo pamoja na kuwasisitiza wazazi kuwapeleka watoto kwenye vituo vya afya ili kupata huduma ya chanjo.
Akizindua Maadhimisho hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mkuu wa wilaya ya Lindi, Dr Nasor Ally Hamid alieleza kuwa Mpango utakaosaidia kutokomeza magonjwa kama vile kifua kikuu, kifaduro, polio, nimonia, pepopunda, homa ya ini na uti wa mgongo pamoja na kuzuia vifo vya watoto
Pamoja na kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kwa kiasi kikubwacha
kuwapatia chanjo watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja kwa zaidi ya asilimia 80 ambao wako katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa hayo, Wito umetolewa Kwa Akina Mama kujitokeza kupata chanjo hizo kufuatia kubainika kuwa watoto hawajapata chanjo na wengine kutokamilisha chanjo hizo.
Akiongelea Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Okoa maisha, jikinge na ulemavu Pata chanjo”. Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dr Sonda Yusuf Shaban alizitaka Halmashauri kuongeza ununuzi wa gesi na majokofu ili kusaidia uzuiaji wa magonjwa kupitia chanjo mbalimbali Sambamba na Uzinduzi huo Mratibu wa Chanjo Mkoa, Bi Zainab Mathradas alitoa wito kwa akina mama kuacha kuzalia Nyumbani ikiwa pamoja na akina baba kuhudhuria Kliniki kwa Vipimo mbalimbali ambavyo vimeanza kutolewa sambamba na akina mama wajawazito
Mkoa wa Lindi una jumla vituo 238 vya huduma ambapo kati ya hivyo ni 197 tu vinavyotoa huduma za chanjo kiwango cha utoaji huduma hiyo ikiongezeka kwa asilimia 7 na kuvuka lengo la kitaifa kwa asilimia 98 badala ya 80 iliyopangwa.
Tags
HABARI ZA KITAIFA